Habari

RAIS DK.MWINYI AKUTANA NA DK.BARBEL KOFLER JIJINI BERLIN

0:00

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiendelea na ziara yake nchini Ujerumani leo Jumatatu Juni 19, 2023 amekutana na Dk.Barbel Kofler , Katibu wa Bunge upande wa Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo Ujerumani.

Mazungumzo yao yalijikita zaidi kuimarisha uhusiano uliopo baina ya Tanzania hasa Zanzibar kwa upande mmoja na Ujerumani.

Rais Dk. Mwinyi alimweleza Dk.Kofler maeneo matatu ambayo Zanzibar ingependa zaidi kushirikiana na Ujerumani ikiwemo nchi hiyo kusaidia miradi ya maji, michezo na afya vilevile namba ya kujenga misingi ya kuimarisha usimamizi wa matumizi ya fedha za miradi.

Naye , Dk.Kofler amempongeza Rais Dk.Mwinyi kwa kuwa na mawaziri sita Wanawake hali inayoonesha kuwaongezea uwezo zaidi Wanawake na Mhe.Rais Dk.Mwinyi akamhakikishia Dk.Kofler kwamba viongozi Wanawake aliowateua kushika nyadhifa mbalimbali wanafanya kazi nzuri na huenda akawapa wengi nafasi zaidi.

Back to top button