Uchumi

DK.MWINYI AFUNGUA JUKWAA LA UVUVI KATI YA KOREA NA AFRIKA

0:00

 Leo,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Hussein Ali Mwinyi amefungua Mkutano wa Tisa wa Jukwaa la Uvuvi baina ya Korea na Nchi za Afrika(KORAFF 2023) uliyofanyika Hoteli ya Golden Tulip Airport.

Dk. Mwinyi amesema Tanzania ina fursa nyingi za biashara, uwekezaji na utalii hivyo ameiomba Korea kuwekeza kwenye sekta ya Uchumi wa Buluu kupitia sekta ya bahari.

Vilevile Serikali imeikaribisha Korea kuwekeza kwenye ujenzi na matengenezo ya meli katika bandari jumuishi ya Mangapwani.

Naye , Rais wa Taasisi ya bahari Korea , Dk.Kim Jong-Deog amesema Tanzania na Korea zimekua na ushirikiano mzuri kwenye sekta za uvuvi na Uchumi wa Buluu.

Back to top button