Vijana Na Michezo
Mawaziri wa Mambo ya Ndani na Michezo wakubaliana kuongeza idadi ya watu katika fainali ya Ligi ya Mabingwa ya CAF
Mervet Sakr

Waziri wa Michezo akizungumza na Mkuu wa Klabu ya Al-Ahly kwa ajili ya Uratibu
Waziri wa Vijana na Michezo, Dkt. Ashraf Sobhy, na Meja Jenerali Mahmoud Tawfik, Waziri wa Mambo ya Ndani, walikubaliana kuongeza idadi ya mashabiki wa Misri watakaoshuhudia fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya klabu ya Misri ya Al-Ahly na klabu ya Wydad ya Morocco.
Mawaziri hao wawili pia walikubaliana kuwa ongezeko hilo litafanyikwa kwa mujibu wa kanuni zinazosimamia mchakato wa mahudhurio ya umma na kwa mujibu wa vigezo na masharti kadhaa.
Waziri huyo wa Vijana na Michezo alifanya mazungumzo ya simu na Kocha Mahmoud Al-Khatib, Mkuu wa Klabu ya Al-Ahly, kuratibu suala hilo.










