Habari
Mazungumzo ya Misri-Uingereza kuhusu Afrika

Balozi Hamdy Sanad Loza, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kwa Masuala ya Afrika alipokea, jana Mei 25, 2023, Mbunge Andrew Mitchell, Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa na Afrika huko Uingereza.
Mazungumzo hayo yalishughulikia mahusiano ya pamoja kati ya nchi hizo mbili na njia za kuyaimarisha, na maandalizi ya Uingereza kwa mkutano wa pili wa uwekezaji kati ya Uingereza na Afrika uliopangwa kufanyikwa 2024; tena walibadilishana maono na maoni juu ya masuala kadhaa ya kimataifa na kikanda ya maslahi ya pamoja, ikiwa ni pamoja na maendeleo nchini Sudan na Syria, na athari za mgogoro wa Ukraine kwa nchi za Afrika.










