Chuo kikuu cha Taifa Zanizbar (SUZA) kimendaa mafunzo ya siku tatu ya teknologia ya habari

Chuo kikuu cha Taifa Zanizbar (SUZA) kimendaa mafunzo ya siku tatu ya teknologia ya habari kwa washiriki kutoka sehemu mbali mbali za Tanzania.

Mafunzo haya ya Bootcamp yaliyoanza jana tarehe 25 na kumalizika taehe 27 mwezi huu ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Hubiquitous unaotekelezwa na DTBi na Chuo cha SUZA yanayofanika katika ukumbi wa Westex Lab katika kampasi ya SUZA Tunguu, Zanzibar.
Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Kompyuta na Teknologia ya Habari katika Chuo cha SUZA Dkt. Omar Haji Kombo amesema mafunzo hayo ya Bootcamp dhamira yake kuu ni kuibua vipaji na kuviendeleza kupitia mradi huo ili kutoa fursa kwa washitiki kuibua vipaji vyao na kuviendeleza kutoka mawazo na kuwa uhalisia ambapo yatatumika kama huduma au bidhaa kwa jamii ili kuendana na mabadiliko ya teknologia na fursa zake kwa wataalamu mbalimbali wa Tehama.

Vile vile, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni tanzu ya Dar Es Salaam ya Tehama (DTBi) DTBI Dkt. Erasto Mlyuka amewataka washiriki wote kuwa na moyo, shauku ya ubunifu na kuyaibua mawazo yao na kuyawasilisha sehemu husika kwani yanaweza kutimiza ndoto zao pamoja na kutatua changamoto kwa jamii zetu katika tasnia ya teknologia.
Awali mafunzo hayo yalitangzwa na chuo cha SUZA na kupatikana maombi zaidi ya 50 na kuchujwa na kupatikana washiriki 32, ambapo kwa sasa wanashiriki mafuno haya.










