Habari Tofauti

Ofisi ya Makamu wa Rais imetoa mafunzo ya kustaafu kwa watumishi wa kada mbalimbali jijini Mwanza

Ofisi ya Makamu wa Rais imetoa mafunzo ya kustaafu kwa watumishi wa kada mbalimbali jijini Mwanza kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kufahamu taratibu za kisheria za kustaafu kazi.

Mafunzo hayo yaliyoanza Mei 23 na kutarajiwa kuhitimishwa Mei 26, 2023 yatawawezesha watumishi hao kutambua stahiki na haki za mtumishi kabla, wakati na baada ya kustaafu.

Pia, watumishi wanaopata mafunzo hayo watapata uelewa wa menejimenti ya mafao ya hitimisho la ajira, ushughulikiaji sahihi wa mirathi ya watumishi, Bima ya Afya baada ya kustaafu.

Ili kukabiliana na msongo wa mawazo wakati wa kustaafu, watumishi hao wamepewa mbinu za kukabiliana na changamoto hiyo pamoja na mbinu za ujasiliamali, biashara na kujikimu kabla na baada ya kustaafu kazi.

Aidha, wastaafu hao wataarajiwa wamefundishwa mbinu za kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza na namna ya maisha kabla na baada ya kustaafu na uandishi sahihi na menejimenti ya wosia.

Mada hizo kwa namna moja au nyingine zitawasidia wastaafu katika utelelezaji wa majukumu yao ya maisha baada ya kustaafu ili kufikia malengo na ndoto zao za maisha baada ya ajira.

Hata hivyo,washiriki hao  wametakiwa kupitia kumbukumbu zao za taarifa ya utumishi ili kubaini iwapo michango imewasilishwa kwenye Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSSSF na kufuatilia taarifa za malipo kwa ajili ya kupata uhakika wa michango yao iwapo inapelekwa.

Hivyo, endapo watabaini mapungufu wawasiliane na Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu ili kutafuta utatuzi wake kabla ya kufikia muda wa kustaafu ili iwe rahisi kulipwa mafao kwa usahihi na kwa wakati.

Back to top button