Habari Tofauti

DK.MWINYI AENDELEA NA ZIARA KUKAGUA MALI ZA CCM  NA JUMUIYA ZAKE ZNZ

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi leo ameendelea na  ziara ya kukagua mali zinazomilikiwa na Chama Cha  Mapinduzi(CCM) na jumuiya zake Zanzibar ikiwemo eneo la  Amani CCM Mkoa, eneo la biashara  la Wilaya  Amani nyuma kwa Wazee, maeneo ya ofisi za  CCM Wilaya ya Amani, miradi ya CCM ofisi ya Wilaya Mjini , kituo cha mafuta kijangwani, miradi ya maduka ya  UVCCM eneo la Darajani , eneo  la Afisi  kuu za UVCCM Gymkhana  Mkoa wa Mjini Magharibi.

Huu ni mwendelezo wa ziara ya kukagua mali zinazomilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) na jumuiya zake inatoa fursa ya kufuatilia na kuboresha utendaji wa mali za Chama ili ziweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kuleta matokeo mazuri kwa Chama  na jumuiya  zake  kujiendesha kiuchumi .

Kwa lengo la kuhakikisha mali za Chama zinaendeshwa na zinafaidisha Chama na jumuiya zake kwa ujumla Zanzibar.

Back to top button