Habari Tofauti

DK.MWINYI AANZA KUKAGUA MALI ZA CCM , ASISITIZA UHAKIKI WA MALI ZA CCM  KWA NGAZI ZOTE ZANZIBAR

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi leo amefanya ziara ya kukagua mali zinazomilikiwa na Chama Cha  Mapinduzi(CCM) Zanzibar ikiwemo eneo la  tawi la CCM Mbweni, ukumbi wa CCM Maisara Social Hall , nyumba ya CCM kumbukumbu ya Afro Shiraz eneo la Posta Kijangwani pia alikutana na familia ya Hayati Nahoda ambao wanaoishi eneo hilo na mwisho kituo cha mafuta  Kinazini Mkoa wa Mjini Magharibi.

Huu ni mwendelezo wa ziara ya kukagua mali zinazomilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa ngazi zote.

Dk.Mwinyi amesema baada ya muda mfupi miradi yote ya uwekezaji itaanza  kwa fursa zilizopo kwenye miradi hiyo  kwa uendelezaji  pamoja na maboresho ya ofisi za  CCM.

 

Back to top button