Habari Tofauti

Kumbukumbu ya Muungano wa Jamhuri ya Tanzania

Tarehe 26 Aprili ya kila mwaka ni siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Jina la “Tanzania” linatokana na kuunganishwa kwa majina mawili nayo ni Tanganyika ( sehemu ya bara) na Zanzibar (mkusanyiko wa visiwa vilivyoko kwenye Bahari kuu ya Hindi) vilivyounganishwa mnamo 1964.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanzishwa mnamo Aprili 26, 1964, kama muungano baina ya nchi mbili huru nazo ni: Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri maarufu ya Zanzibar,  zilizofanya mkataba wa muungano uliotiwa saini na Rais “Julius Nyerere” Rais wa zamani wa Jamhuri ya Tanganyika na Sheikh “Abeid Amani Karume” Rais wa zamani wa Jamhuri ya Zanzibar mnamo Aprili 22, 1964, huko kisiwani Zanzibar.

Mkataba huo uliidhinishwa na Baraza la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi mnamo  Aprili 26, mwaka huo huo na hivyo Rais “Julius Nyerere” akawa Rais wa kwanza wa Tanzania na Sheikh “Abeid Karume” akawa Makamu wa Kwanza wa Rais.

Tanganyika ilipata uhuru wake kutoka kwa udhibiti wa Uingereza mnamo Desemba 9, mwaka1961, tena jimbo la Zanzibar likapata uhuru kutoka kwa Uingereza mnamo Desemba 19 mwaka1963,Kisha Tanganyika ikaungana na Zanzibar mnamo  Aprili 26, 1964 na kuunda pamoja Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ambayo jina lake lilibadilishwa tena mnamo Oktoba 29 ya mwaka huo huo na kuwa jina la sasa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Muungano huo wa Tanganyika na Zanzibar ulianzishwa kwa sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mahusiano ya kina na ya kihistoria baina ya nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali pamoja na mwingiliano wa kijamii, utamaduni na lugha, ushirikiano wa kisiasa wa muda mrefu baina ya Muungano wa Kitaifa wa Tanganyika (TANU) na Chama cha Afro-Shirazi (ASP), pamoja na ushirikiano wa muda mrefu baina ya watu na viongozi wakati wa harakati ya kitaifa iliyosababisha uhuru wa nchi hizo mbili, na miongoni mwa sababu muhimu za kuanzishwa kwa Muungano huo pia ni utashi wa kuwepo kwa Muungano wa Bara la Afrika, basi Rais “Julius Nyerere” na viongozi wengine wa Harakati za ukombozi na uhuru Barani Afrika walitamani sana kuwepo kwa Umoja wa Afrika. Hivyo, kwa mara ya kwanza  Barani Afrika, iliwezekana kuunganisha nchi mbili huru, na imethibitika kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ndio Umoja ambao bado upo miongoni mwa Miungano  nadra Ulimwenguni.

Back to top button