Habari Tofauti

Mwenge wa Uhuru umezindua mradi wa maji Mbinga

Ahmed Hassan

 

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ndg. Abdalla Shaibu Karim amezindua  mradi wa  maji katika kata za Bethlehem, Ruhuwiko na Matarawe  katika Halmashauri ya mji wa Mbinga.

Mradi huo umetekelezwa   na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA).

Mradi umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 1,546,248,565.09 na unanufaisha zaidi ya wakazi 12,000.

Back to top button