Habari

RAIS DKT.MWINYI AHITIMISHA KUFUTARISHA MAKUNDI MAALUMU MIKOA YA UNGUJA NA PEMBA

Ahmed Hassan

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaji DkT.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mama Mariam Mwinyi amefutari pamoja na Yatima, Walimu wa Madrasa ,Masheikh , Wajane ,Walemavu na Wazee wa Mkoa wa Kaskazini Pemba leo tarehe 12 Aprili 2023 ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba. .
Aidha, Rais Alhaji Dk.Mwinyi amehitimisha kufuturisha katika Mikoa ya Unguja na Pemba leo Mkoa wa Kaskazini Pemba kwa makundi maalumu Mikoa yote .

Vilevile, DkT.Mwinyi amewahimiza waumini wa dini ya Kiislamu kuongeza jitihada kwa kufanya ibada katika kumi la Mwisho kwa Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani.
Back to top button