Habari

Rais El- Sisi aangalia maendeleo ya kazi katika Bwawa la Julius Nyerere nchini Tanzania

Mervet Sakr

Rais Abdel Fattah El-Sisi amekutana leo na Waziri Mkuu Dkt. Mostafa Madbouly na Waziri wa Nyumba, Huduma na Jamii za Mijini Dkt. Assem El-Gazzar.

Mshauri Ahmed Fahmy, Msemaji Rasmi wa Urais wa Misri, alieleza kuwa Rais alipewa taarifa wakati wa mkutano huo kuhusu maendeleo ya kazi katika Bwawa la Julius Nyerere la kuzalisha Umeme kwa maji nchini Tanzania, unaotekelezwa na Muungano wa Arab Contractors na El-Sewedy Electric pamoja na usimamizi wa Serikali ya Misri, nao ni mradi mkubwa zaidi wa maendeleo unaotekelezwa katika ngazi ya Tanzania, kwani unachangia kuzalisha mara mbili ya kiasi cha nishati inayopatikana nchini kwa sasa, na hivyo, inawakilisha mfano wa kufuatwa katika ushirikiano wenye matunda, ambao Misri inaupenda na ndugu zake wa Kiafrika, kuelekea ujenzi na maendeleo kwa manufaa ya waafrika wote.

Mkutano huo pia ulishughulikia hali ya kazi inayoendelea katika miji kadhaa mipya, ikiwa ni pamoja na Mji Mkuu Mpya wa Utawala na Jiji Jipya la Alamein, pamoja na kufuatilia miradi mingi ya kuendeleza eneo la kihistoria la Kairo, ndani ya muktadha wa juhudi za serikali za kufikia ushirikiano endelevu kati ya kisasa na maendeleo nchini kote, pamoja na kurejesha sura nzuri ya kiustaarabu ya Kairo, na kuhifadhi tabia maalum ya maeneo yote ya thamani ya kihistoria katika ngazi ya Jamhuri.

Msemaji huyo alihitimisha hotuba yake kwa kueleza kuwa Rais Abdel Fattah El-Sisi pia alifahamishwa juu ya maendeleo ya hivi karibuni katika mradi wa “Mabadiliko Makubwa juu ya Ardhi ya Amani” katika jiji la Mtakatifu Catherine huko Sinai, ambapo alielekeza katika suala hili kuzingatia maelezo yote ya mradi huo, ili eneo hili la kipekee liwe kivutio cha kimataifa kwa wageni kutoka Duniani kote, kwa kuendelea na utekelezaji wa mradi huo jumuishi, unaozingatia viwango vya kimataifa vya uendelevu wa mazingira, kuhifadhi urithi wa usanifu, na kuongeza thamani ya kiroho, kwa eneo hilo, kama mahali pa kukutana dini tofauti na nchi ya Amani.

Back to top button