Habari

Rais wa Zanzibar ametunukiwa Tuzo ya VIP Global Water Changemakers Awards

Ahmed Hassan

0:00

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ametunukiwa Tuzo maalumu ijulikanayo kama VIP Global Water Changemakers Awards kutokana na jitihada zake za kuifanya Zanzibar kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuanzisha na kuzindua programu ya uwekezaji katika sekta ya maji.

Tuzo hiyo imetolewa wakati wa mkutano wa maji wa Umoja wa Mataifa tarehe: 22 Machi 2023 jijini New York, Marekani.

Tuzo hiyo ya Kimataifa ya Mabadiliko ya Sekta ya Maji atakabidhiwa rasmi Rais Dk. Mwinyi kesho tarehe: 05 Aprili 2023, saa 3 asubuhi.

Back to top button