Habari Tofauti

Rais El Sisi ashuhudia sehemu ya vipimo vya waombaji kujiunga na nyadhifa za Wizara ya Ulezi, Elimu na Elimu ya Ufundi

Mervet Sakr

0:00

Rais Abdel Fattah El-Sisi alishuhudia sehemu ya mitihani kwa waombaji kujiunga na Nyadhifa za Wizara ya Elimu na Elimu ya Ufundi, inayofanyika kwa ushirikiano na Chuo cha Kijeshi cha Misri, kwa mahudhurio ya Jenerali Mohamed Zaki, Waziri wa Ulinzi na Uzalishaji wa Kijeshi, Dkt. Reda Hegazy, Waziri wa Elimu na Elimu ya Ufundi, na Luteni Jenerali Ashraf Salem Zaher, Mkurugenzi wa Chuo cha Kijeshi cha Misri.

Mshauri Ahmed Fahmy, Msemaji Rasmi wa Urais wa Misri, alisema kuwa Rais alipewa taarifa kuhusu mfumo wa usajili wa matokeo ya vipimo kwa njia ya kielektroniki, unaofuatilia taarifa za waombaji, na matokeo waliyoyapata wakati wakifanya hatua mbalimbali za vipimo, hadi walipofikia hatua ya mwisho. Pia alifanya mazungumzo na waombaji, ili kufahamu kuhusu dira na mawazo yao kuhusu ajira wanazoomba, na jitihada zinazoendelea za kufikia maendeleo katika sekta zote nchini.

Msemaji huyo aliongeza kuwa Rais alithibitisha nia ya serikali kufuata viwango vya juu vya kisayansi na kiufundi ili kuchagua vipengele bora na kada za binadamu kwa ajili ya ajira za umma, baada ya kupitisha mafunzo ya kina na sifa zilizoandaliwa na wataalamu, sambamba na asili ya kazi zao na ajira zilizotumika kwao, ndani ya muktadha wa dira ya serikali ya kuendeleza kiwango cha utendaji wa serikali na kuweka mazingira mwafaka ya kuachia uwezo wa vijana, na kuwapa mazingira yanayofaa kisayansi, kiteknolojia na kitaaluma katika ngazi zote, kwa namna inayochangia kuboresha kiwango cha huduma za umma zinazotolewa kwa watu wa Misri.

Back to top button