Habari

RAIS DK.MWINYI AKUTANA NA BALOZI WA UINGEREZA NCHINI TANZANIA

Ahmed Hassan

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mh.David Concar kwa mazungumzo leo tarehe 30 Machi 2023 Ikulu, Zanzibar .
Mazungumzo yao kwa kiasi kikubwa yaligusia ujenzi wa uwanja mpya wa ndege wa Pemba ambapo Balozi huyo wa Uingereza alimwambia Mhe.Rais suala la mchakato wa fedha wa mradi huo unakwenda vizuri.
Uingereza ni mshirika mkubwa katika ujenzi wa mradi huo wa Pemba.
Back to top button