Habari Tofauti

Dkt. Swailem ashiriki katika kikao cha “Mpango wa Timu ya Ulaya .. Kuunganisha juhudi za usimamizi wa pamoja wa maji Barani Afrika”

Mervet Sakr

Prof.Hany Sweilam, Waziri wa Rasilimali za Maji na Umwagiliaji na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Maji Afrika (AMCAO), walishiriki katika kikao cha “Mpango wa Timu ya Ulaya… Kuunganisha juhudi za usimamizi wa pamoja wa maji Barani Afrika”, katika Mkutano wa Mapitio ya Muda wa Kati wa Umoja wa Mataifa huko New York.

Dkt. Swailem alitoa hotuba yake kwa nafasi yake kama Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Maji Afrika (AMCAO) ambapo alizungumzia changamoto zilizopo sasa zinazoikabili sekta ya maji katika ngazi ya kimataifa, na haja ya kuzingatia umakini katika usimamizi wa maji na ushirikiano katika usimamizi wa pamoja wa maji kama kipengele muhimu katika kuendeleza maendeleo ya kijamii na kiuchumi, akibainisha kuwa Ajenda ya Umoja wa Afrika ya mwaka 2063 “Afrika tunayoitaka” haiwezi kufikiwa bila usimamizi endelevu wa maji ya pamoja, na kufikia malengo yetu ya bara na kimataifa juu ya mahitaji ya maji, uratibu mzuri na ushirikiano ni muhimu katika kuboresha usimamizi wa maji.

Tena amesifu mpango wa Timu ya Ulaya kwa Usimamizi wa Maji ya pamoja, ambao kutokana na umuhimu wake katika ngazi za kitaifa, kikanda na bara, Halmashauri Kuu ya Baraza la AMCAO ilichukua uamuzi wa kuiagiza Sekretarieti kukamilisha “hati ya kazi” ya mpango huo kulingana na Mkakati wa AMCAO 2018-2023, na kuzindua mchakato wa mashauriano ya kuendeleza maono ya Afrika ya mpango huo ili kuhakikisha kuwa maslahi ya nchi zote za Afrika yanazingatiwa na kuchangia kukuza maendeleo endelevu ya bara hilo na kukuza amani na usalama kote Afrika.

Mpango huo pia umeunganishwa sana na mipango kadhaa inayoendelea ikiwa ni pamoja na Mpango wa Kukabiliana na Sekta ya Maji (AWARe), unaolenga kuchochea ushirikiano wa kina katika nyanja ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, akibainisha kuwa utaratibu wa utekelezaji wa mipango yote miwili unapaswa kuonesha umuhimu wa ushirikiano katika usimamizi wa pamoja wa maji, kuimarisha fedha, kubadilishana maarifa, kujenga uwezo, teknolojia na ubunifu ili kupata matokeo yanayotarajiwa.

Back to top button