Habari

Waziri Mkuu akagua Jengo jipya la Halmashauri ya Mji wa Bariadi

Ahmed Hassan

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Leo Machi 24, 2023 amekagua Jengo jipya la Halmashauri ya Mji wa Bariadi ambalo limefikia asilimia 95 ya ujenzi na lina thamani ya bilioni 3.
Jengo hilo limeanza kutumika kwa baadhi ya vitengo vya halmashauri linatarajiwa kurahisisha utoaji wa huduma za serikali kwa wananchi wa halmashauri ya bariadi.
Baada ya ukaguzi huo Waziri Mkuu anafanya kikao na watumishi wa Halmashauri za Mkoa wa Simiyu.
Back to top button