Habari
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Masuala ya Afrika apokea Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Zambia
Mervet Sakr
Balozi Hamdi Sanad Loza, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Masuala ya Afrika, amempokea Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Zambia, Bw. Chimbo Mbula, akiwa ameambatana na Balozi wa Zambia jijini Kairo, na Mkurugenzi wa Taasisi ya Diplomasia ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Zambia, kwa kumshirikisha Balozi Walid Haggag, Mkurugenzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Diplomasia katika Wizara ya Mambo ya Nje.
Mkutano huo ulishughulikia njia za kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizo mbili, hasau katika nyanja za biashara na uwekezaji, zilizokuwa zikishuhudia ukuaji thabiti mnamo miaka ya hivi karibuni, na kuimarisha uratibu kati ya nchi hizo mbili katika majukwaa ya Kiafrika na kimataifa.