Habari

RAIS DK.MWINYI AKUTANA NA WAWEKEZAJI KUTOKA UINGEREZA

Ahmed Hassan

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar imefungua milango ya Uwekezaji.

Aliyasema hayo alipokutana na Wawekezaji kutoka Uingereza ambao waliongozwa na Bi. Agnes Gitau kutoka Taasisi ya Eastern Africa Association pamoja na Amanda Van Dyke wa Kampuni ya ARCH, leo tarehe 23 Machi 2023 Ikulu Zanzibar.

Vilevile ,Rais Dk.Mwinyi amewataka Wawekezaji hao kuwekeza katika fursa zitokanazo na Uchumi wa Buluu na zaidi kwenye suala la uvuvi na vifaa vya kuhifadhia samaki .

Back to top button