Vijana Na Michezo

Refa 7 wa Misri katika kambi ya Umoja wa Afrika

Mervet Sakr

Kamati kuu ya Refa ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) ilitangaza uteuzi wa timu ya Refa wa Misri katika kambi ya Refa wasomi Barani Afrika; kushiriki katika kozi ya maandalizi ya wasomi kabla ya robo fainali ya Kombe la Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho kwa msimu huu.

De Nomandes wa Ivory Coast, mkurugenzi wa Kamati ya Refa wa CAF, alichagua wafanyakazi wa Misri waliowakilishwa na Amin Omar na Mohamed Maarouf kama waamuzi katika orodha ya Refa waliopewa jukumu la kusimamia mechi za raundi ya mwisho kwenye Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho, na Mahmoud Abu Al-Rejal na Ahmed Hossam Taha wakiwa miongoni mwa orodha ya Refa wasaidizi, huku Mahmoud Ashour, Ahmed Al-Ghandour na Amr El-Shenawy wakichaguliwa miongoni mwa orodha ya Refa wa VAR.

Refa wanaoshiriki kambini wamepangiwa kufanya vipimo vya kimwili na kinadharia na vikao vya vitendo mnamo kipindi cha mazoezi, na endapo mtihani utashindikana kwa Refa yeyote, atatengwa katika raundi za mwisho rasmi na kwa uhakika bila kufanya mchezo wowote wa marudiano.

Kamati ya Refa ya CAF iliamua kuandaa mashindano hayo nchini Misri kuanzia Aprili 14 hadi 18 na kuweka Aprili 13 kama tarehe ya mwisho kwa Refa kufikia Kairo.

Back to top button