Habari Tofauti

RAIS DK.MWINYI AWATAKA WATAALAMU WA LUGHA YA KISWAHILI KUCHANGAMKIA FURSA DUNIANI

Ahmed Hassan

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi ametoa rai kwa wataalamu wa lugha ya kiswahili wakiwemo wahadhiri ,walimu ,waandishi wa habari,watangazaji na wakalimani kuchangamkia fursa zilizopo kupitia Kiswahili zinazoendelea kuongezeka duniani. Aliyasema hayo alipofungua Kongamano la Idhaa za Kiswahili kwa Mwaka 2023, lililofanyika leo tarehe 18 Machi 2023 ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-Wakil.

Aidha, Dk.Mwinyi amesema lugha ya Kiswahili inaendelea kukua na kuwa ni bidhaa muhimu ya mawasiliano kimataifa. Hata hivyo bado inaonekana mwamko mdogo kwa watu katika kuzichangamkia fursa zilizopo.

Back to top button