Habari

RAIS DKT. MWINYI AKUTANA NA WAWEKEZAJI KUTOKA KOREA

Ahmed Hassan

0:00

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amekutana na ujumbe kutoka kampuni ya Global Cooperation Committee (GCC) ukiongozwa na Mwenyekiti wao Bw. Jin-il, Kim.
Rais Dkt. Mwinyi amewakaribisha wawekezaji hao na kuahidi kuwa Zanzibar ipo tayari hususan katika sekta ya Utalii na Uchumi wa buluu.
Naye, Bw. Kim Mwenyekiti wa GCC amesema wapo tayari kushirikiana na Zanzibar kwa kuanzisha Kiwanda cha kusarifu samaki na pia kuleta wataalamu waliobebea katika sekta ya uvuvi kutoka Korea.
Back to top button