Habari

RAIS DKT.MWINYI AVITAKA VIKUNDI VYA MAZOEZI  KUIBUA FURSA ZA MIRADI YA UJASIAMALI NA KUSAFISHA MAZINGIRA

Ahmed Hassan

0:00

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi awapongeza Chama cha Mchezo wa Mazoezi ya Viungo Zanzibar (ZABESA), kwa utaratibu wa kuwaunganisha wananchi kwa kufanya Mazoezi kwa kuimarisha afya za watu , kuwaweka pamoja kwani umoja wao unaweza kuleta tija  kwa maendeleo katika kuibua fursa mbalimbali  kwa vikundi hivyo .

Rais Dkt.Mwinyi aliyasema hayo alipokutana na Uongozi wa Chama cha Mchezo wa Mazoezi ya Viungo Zanzibar (ZABESA) , ukiongozwa na Mwenyekiti wake  Said Suleiman  Said.

Dkt.Mwinyi amesema hamasa inayotolewa katika ufanyajaji Mazoezi ni njia sahihi katika kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni hamasa yenye tija, pia amewaasa kuendelea kuwashawishi wananchi zaidi waendelee kujiunga katika vikundi hivyo walio katika vikundi wasitoke.

Rais Dkt.Mwinyi amewaunga mkono na kuwapongeza kwa  utaratibu wa kufanya usafi katika kisiwa cha Changuu na ameunga mkono wazo la Siku ya Jumamosi kuwa siku ya usafi   na ameshauri ili vikundi viwe kimaendeleo zaidi katika Uanzishwaji wa shughuli za uzalishaji mali  kwa maana inakuwa rahisi kwa Serikali kuwasaidia wakiwa katika vikundi .

Dkt.Mwinyi amewataka ZABESA kushirikiana na sekta binafsi hasa makampuni ya simu na benki kufanikisha matamasha yao  kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu ufanyajaji Mazoezi na usafi wa Mazingira  .

Dkt.Mwinyi amewaahidi kushirikiana nao  kutafuta waatalamu wa Mazoezi  ambao watakuwa watajitolea kufundisha vikundi mbalimbali  aina za ufanyaji wa Mazoezi.

Naye , Mwenyekiti  wa chama hicho ndugu Said amempongeza  Rais Dk.Mwinyi kwa kutimiza miaka miwili ya Uongozi wake kwa Maendeleo anayowaletea Wazanzibari , pia kwa kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar.

Ndugu Said , amesema wataunga mkono juhudi za Serikali  na kubuni miradi mbalimbali mbadala ya kuhifadhi takataka .

Alisema ZABESA imejipanga kuungana na Dunia kuadhimisha siku ya Usafi Duniani  inayo adhimishwa kila Jumamosi  ya tatu ya Mwezi wa Septemba kila Mwaka.

Vile vile, wamesema ZABESA ina lengo la kugeuza mtazamo wa kimazoezi na uwe Mazoezi kwa afya na maendeleo  tofauti kwa sasa.

Back to top button