
Mheshimiwa Prof. Mohamed Mokhtar Gomaa, Waziri wa Awqaf, alishiriki katika mkutano wa Kamati ya Masuala ya Afrika ya Baraza la Wawakilishi, Jumatatu, 13/2/2023, iliyoongozwa na Dkt. Sherif Al-Gabali na mbele ya wajumbe kadhaa wa Kamati ya Masuala ya Afrika ya Baraza la Wawakilishi, kujadili jukumu na juhudi za Wizara hiyo ya Awqaf Barani Afrika, na kueneza uelewa wa kidini kupambana na mikondo ya itikadi kali katika ngazi ya Bara la Afrika.
Wakati wa hotuba yake, Prof. Mohamed Mokhtar Gomaa, Waziri wa Awqaf, alisisitiza kuwa jukumu la taasisi za kitaifa limeunganishwa ili kusaidia jukumu kubwa la Misri Barani Afrika na Duniani kote, akisisitiza kuwa Afrika ni kina muhimu cha kimkakati, na katika mkutano huo, Prof. Mohamed Mokhtar Gomaa, Waziri wa Awqaf, aliwasilisha juhudi muhimu zaidi za Wizara hiyo Barani Afrika, ambazo muhimu zaidi ni:
Kwanza: Katika uwanja wa kupeleka Idadi ya wajumbe katika nchi za Afrika kwa sura ya daima ni maimamu, wahubiri na walimu 27 : ambapo idadi ya wajumbe wa kudumu wa Tanzania ilifikia wajumbe (12), huko Senegal (4), huko Uganda (3), huko Msumbiji (3), huko Cameroon (2), na huko Kenya (2), na mjumbe mmoja huko Sudan, pamoja na kutuma baadhi ya wasomaji na maimamu wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Pili: Katika uwanja wa mikutano ya kimataifa
Baadhi ya wawakilishi wa nchi za Afrika, wakiwemo mawaziri, mufti na wakuu wa mabaraza, walialikwa kushiriki katika mikutano miwili ya kimataifa iliyofanyikwa na Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu wakati wa mwaka 2022, na ushiriki huo ulikuwa kama ifuatavyo:
1- Mkutano Mkuu wa 32 wa Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu ukiwa na kichwa: (Mkataba wa Uraia na Athari zake katika Kufikia Jumuiya na Amani ya Kimataifa) kuanzia tarehe 12 hadi 13 Februari 2022, kwa kushirikisha wawakilishi wa Nchi 20 za Afrika, nazo ni (Tunisia – Algeria – Djibouti – Gambia – Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo – Comoro – Uganda – Zambia – Rwanda – Ghana – Cameroon – Sudan Kusini – Guinea Conakry – Tanzania – Chad – Msumbiji – Côte d’Ivoire – Kenya – Burundi – Senegal).
2- Mkutano Mkuu wa 33 wa Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu ukiwa na kichwa: (Jitihada ni muhimu sana kwa zama hii “Sura zake – kanuni zake – wafuasi wake – uhitaji kwake”) mnamo kipindi cha kuanzia tarehe 24 hadi 25 Septemba 2022, kwa kushirikisha wawakilishi kadhaa wa nchi za Afrika, yaani: (Tunisia – Algeria – Madagascar – Sudan – Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo – Morocco – Uganda – Zambia – Rwanda – Cameroon – Sudan Kusini – Nigeria – Msumbiji – Côte d’Ivoire – Libya – Burundi – Senegal – Malawi – Burkina Faso – Mauritania – Benin).
3- Kushiriki katika Mkutano wa Afrika wa Kukuza Amani ukiwa na kichwa: “Shirikini wote katika Amani” huko Mauritania, Januari 2023.
Tatu: Ushindani wa Kimataifa wa Quran Tukufu
Mashindano ya 29 ya Kimataifa ya Quran Tukufu yaliandaliwa kuanzia tarehe 4 hadi 8 Februari 2023, ambapo nchi 33 zilishiriki kutoka bara la Afrika, na washindani kadhaa walipata nafasi za juu na uwepo wa ajabu katika Mashindano ya Kimataifa ya 29 ya Quran Tukufu, wa kwanza walikuwa:
1. Mshindani/ Abdul Samad Adam kutoka Ghana, ambapo alishinda nafasi ya kwanza katika kitengo cha tano (kukariri Quran Tukufu kwa wasemaji wasio Waarabu) na maksi yake ya 99.90%, na akashinda tuzo ya paundi elfu 200, cheti cha shukrani, nakala ya Al-Montakhab katika tafsiri ya maana ya Quran Tukufu na nakala ya kamusi elezo ya Utamaduni wa Kiislamu.
2. Mshindani / Abdullah Ezz El-Din Abdel Rahman kutoka Sudan, ambapo alishinda nafasi ya pili katika tawi la kwanza (kukariri Qur’ani Tukufu na kuelewa maana yake na madhumuni ya jumla kwa wamiliki wa sauti nzuri) na maksi yake ya 94.85%, na alishinda tuzo ya paundi elfu 150, cheti cha shukrani na nakala ya Al-Montakhab katika tafsiri ya maana ya Qur’ani Tukufu na nakala ya kamusi elezo ya Utamaduni wa Kiislamu.
Washiriki wengi kutoka bara la Afrika pia walifanikiwa kuwepo kwa ajabu, ikiwa ni pamoja na:
1. Mshindani/ Haitham Sakr Ahmed kutoka Kenya, ambapo alishinda nafasi ya nne katika kitengo cha tano (kukariri Quran Tukufu kwa wazungumzaji wasio Waarabu) kwa cheti cha shukrani na nakala ya Al-Montakhab katika tafsiri ya maana ya Quran Tukufu na nakala ya timu kamusi elezo ya Utamaduni wa Kiislamu.
2. Mshindani/ Nafisa Bousso kutoka Senegal, ambapo alishinda nafasi ya saba katika kitengo cha tano (kukariri Quran Tukufu kwa wasemaji wasio Waarabu) akiwa na cheti cha shukrani na nakala ya Al-Montakhab katika tafsiri ya maana ya Quran Tukufu na nakala ya kamusi elezo ya Utamaduni wa Kiislamu.
3. Moaz Dweik kutoka Ufalme wa Morocco pia alivuta watu kwa sauti yake tamu.
Nne: Katika uwanja wa shughuli zinazotolewa kwa wanafunzi wanaotoka nchi za Afrika:
A- Udhamini wa Wanafunzi wa Kimataifa:
Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu limetoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wapatao (100) kutoka nchi za Afrika, kwa gharama ya jumla ya paundi milioni moja laki sita.
B- Kambi za elimu na burudani kwa wanafunzi wa kimataifa:
Kambi 5 za elimu na burudani ziliandaliwa kwa ajili ya wanafunzi wa kimataifa wakati wa 2022 kwa ushiriki wa wanafunzi kutoka nchi za Afrika, na kambi hizo zilijumuisha masuala ya kisayansi, kiutamaduni na burudani na kutembelea vivutio vya utalii na akiolojia huko mkoa wa Alexandria.
C- Mashindano ya Quran kwa wanafunzi wa kimataifa:
1- Mashindano ya Quran Tukufu namba 3 huko Baraza kuu la Masuala ya Kiislamu kwa wanafunzi wageni wanaosoma huko Al Azhar Al Sharief, vyuo vikuu vya kimisri, vyuo vya juu na vyuo vya Al Azhar, mnamo kipindi cha Agosti 2-31, 2022, na hivyo kwa ushiriki wa zaidi ya wanafunzi 30 kutoka nchi za kiafrika, na hivyo ilisababisha kupatia washindi kwa tuzo za kifedha, maktaba kuu kutoka kwa machapisho ya Baraza hilo, nao ni washindi 6, pia kuwashauriwa kujiunga katika tawi la kwanza la ushindani wa kimataifa wa 29 kwa Quran Tukufu nao walikuwa 5.
Tano : katika uwanja wa Maktaba kamilifu zinazotolewa kwa Taasisi na Vituo vya kiislamu huko nje
Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu limetoa zawadi kwa maktaba 13 jumuishi zenye jumla ya nchi mbalimbali za Afrika, na maktaba hizi zilijumuisha machapisho mengi ya Wizara ya Awqaf na Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu na mfululizo (Vision) kwa ajili ya fikra zilizoangaziwa kwa Kiarabu na lugha mbalimbali za kigeni, kwa kila nchi zifuatazo: (Burkina Faso – Mauritania – Tanzania – Sudan – Sudan Kusini – Morocco – Somalia – Algeria – Tunisia – Ghana – Chad – Malawi – Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo).
Sita: Katika uwanja wa kutafsiri na kuchapisha katika lugha mbalimbali za kigeni.
Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu limetafsiri vitabu kadhaa katika lugha za Kiafrika, kama ifuatavyo:
1- Al- Montakhab katika tafsiri ya maana ya Qur’ani Tukufu katika lugha ya (Kihausa).
2- Dhana ambazo lazima zirekebishwe mbele ya itikadi kali kwa lugha ya (Kiswahili).
3- Ufahamu wa makusudi wa Sunnah ya Mtume ( S.A.W) katika lugha ya (Kiswahili).
4- Hatari za ukanaji Mungu na njia za kukabiliana nayo lugha ya (Kiswahili).
Saba: Katika uwanja wa mafunzo katika Chuo cha Kimataifa cha Awqaf.
1. Kikao cha kwanza cha Shirikisho la Utangazaji la Kiislamu chenye kichwa: “Uraia na Jumuiya na Amani ya Kimataifa”, kuanzia 14/5/2022 hadi 24/5/2022, kwa wawakilishi 25 wa vyombo vya habari wanaowakilisha nchi 19 ambapo (Burkina Faso – Chad – Tunisia – Gabon – Gambia – Comoro – Djibouti – Senegal – Sudan – Somalia – Cameroon – Mali – Niger) walishiriki.
2. Kozi ya maimamu na wahubiri wa Burkina Faso, kuanzia 28/5/2022 hadi 7/6/2022, kwa maimamu na wahubiri (20), maimamu 12 na wahubiri wakike 8 kutoka Burkina Faso.
3. Kikao cha pili cha Shirikisho la Utangazaji la Kiislamu chenye kichwa: “Kuishi pamoja kwa Amani na Amani ya Jamii”, kuanzia tarehe 24/9/2022 hadi 4/10/2022, kwa waandishi wa vyombo vya habari 26 vinavyowakilisha nchi 15, na kushiriki ndani yake kutoka nchi za bara la Afrika: (Sudan – Tunisia – Algeria – Gambia – Mauritania – Uganda – Senegal – Benin – Niger),
pamoja na watangazaji kadhaa kutoka Jamhuri ya Kiarabu ya Misri.
4. Kikao cha maimamu na mawakala wa majaliwa katika nchi ndugu ya Algeria mnamo kipindi cha kuanzia 8/ 12/2022 hadi 26/12/2022, kwa watu 19 kutoka Algeria.
5. Kozi ya Maimamu Tanzania, kuanzia tarehe 2/2/2023 hadi 11/2/2023, kwa maimamu 10 kutoka Tanzania.
Nane: Katika uwanja wa ushirikiano na huduma ya jamii ya Afrika
Paundi milioni 20 zilitolewa kama mchango wa misaada ya serikali ya Misri kwa ndugu zetu huko Sudan.
Hiyo ni pamoja na Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sis, kwa kuheshimu baadhi ya viongozi wa dini wa Kiafrika, wakiwemo:
1. Sheikh Shaaban Ramadhani – Mufti wa Uganda mwaka 2018.
2. Dkt. Mohamed Khater Issa – Mkuu wa Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu nchini Chad mwaka 2019.
3. Sheikh Nasr El-Din Mufarreh – Aliyekuwa Waziri wa Masuala ya Kidini na Awqaf nchini Sudan mnamo 2021.
4. Dkt. Abdullah Burj – Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu nchini Sudan Kusini mwaka 2021.
5. Sheikh / Abu Bakr Zubairi Ali – Mufti wa Tanzania mwaka 2022.
Kwa upande wake, Dkt.Sherif El-Gabaly, Mwenyekiti wa Kamati ya Masuala ya Afrika ya Baraza la Wawakilishi, na wajumbe wa Kamati ya Masuala ya Afrika ya Baraza la Wawakilishi alipongeza juhudi za Wizara ya Awqaf ya Misri Barani Afrika, akisisitiza kuwa juhudi hizo zinachangia kusaidia uhusiano wa Misri na kina chake cha Afrika.