Habari Tofauti

Majaliwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu katika Mkoa wa Songwe

Ahmed Hassan

0:00

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu katika Mkoa wa Songwe ambapo akiwa katika kijiji cha Kaloleni kata ya Mkwajuni ameweka jiwe la msingi la hospitali ya wilaya ya Songwe.
 
Ujenzi wa hospitali hiyo ambao umegharimu shilingi bilioni 3.5 mpaka sasa imefikia asilimia 95 ya ujenzi wake ambapo Halmashauri inatarajia kukamilisha Mradi huu tarehe 31machi 2023, ikiwa ni sambamba na kuanza kutumika rasmi kwa majengo yote ambayo tayari vifaa vyake vimepokelewa.
Ujenzi katika hospitali hiyo inahusisha Ujenzi wa Majengo ya huduma za wagonjwa wa nje, Mionzi, Maabara, ufuaji, Famasia, Utawala na Jengo la Mama na Mtoto, Ujenzi wa Wodi tatu za Magonjwa Mchanganyiko.
Majengo mengine ni jengo la Huduma ya dharula na Nyumba ya Watumishi Familia tatu, jengo la Upasuaji, jengo la Uchunguzi na kuhifadhia maiti na wodi mbili za Upasuaji (Wanaume na Wanawake).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara za mji wa Mkwajuni kwa kiwango cha lami.
Ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 1 unatekelezwa kwa kutumia fedha za Mfuko wa Jimbo kiasi cha shilingi milioni 500.
Back to top button