Waziri wa Mambo ya Nje ampokea Mjumbe wa Ulaya kwa ajili ya mchakato wa Amani katika Mashariki ya Kati
Ali Mahmoud
Mheshimiwa Sameh Shoukry, Waziri wa Mambo ya Nje, alipokea Leo, Februari 7, Bw. “Sven Koopmans”, Mjumbe wa Ulaya kwa mchakato wa Amani ya Mashariki ya Kati”.
Katika taarifa za Balozi Ahmed Abu Zeid, Msemaji rasmi na mkurugenzi wa idara ya diplomasia ya umma katika Wizara ya Mambo ya Nje, aliashiria kuwa wakati wa mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje alipitia maendeleo ya hivi karibuni kwenye pande za Palestina na Israeli, na kasi ya kuongezeka kwa ghasia zinazotishia kuondoa hali ya udhibiti, akionya madhara makubwa ya kuendelea kuongezeka kwa usalama na utulivu katika eneo hilo, na kwenye nafasi za suluhisho la nchi hizo mbili.
Katika suala hilo, Waziri wa Mambo ya nje alisisitiza msimamo wa Misri wa ulazima wa kutuliza hali ya mambo ardhini na Israeli iache kuchukua hatua za upande mmoja ambazo zitaongeza hali ya mvutano kati ya watu wa Palestina, kwa sababu ya athari hii ya moja kwa moja katika kujenga mazingira yanayofaa kwa kuanza tena mazungumzo na kurejesha matumaini ya kufikia Amani kamili na ya haki kulingana na suluhisho la nchi hizo mbili kwa mujibu wa maamuzi ya uhalali wa kimataifa.
Shoukry alisisitiza jukumu muhimu ambalo washirika wa kimataifa, wakiongozwa na Umoja wa Ulaya, wanaweza kutekeleza ili kukomesha mvutano wa sasa, kuacha ukiukaji na mashambulizi dhidi ya Wapalestina na kuhimiza pande zote kurudi kwenye mazungumzo.
Balozi Abu Zeid alifunua kwamba mjumbe wa Ulaya alisisitiza nia ya Umoja wa Ulaya kushauriana na kuratibu na Misri kuhusu hali za wasiwasi katika maeneo ya Palestina, na njia na nafasi za kuhamasisha pande za Israeli na Palestina kurejea kwenye mazungumzo kupitia kuwasilisha mapendekezo na maono mapya na ya ubunifu, kwa kuzingatia jukumu muhimu la Misri katika mfumo huu. Mkutano huo ulitoa fursa kwa pande hizo mbili kubadilishana maoni na kuchunguza nafasi za kuchukua hatua mnamo kipindi kinachofuata.
Mzungumzaji wa Wizara ya Mambo ya Nje alihitimisha taarifa zake, akibainisha kuwa mjumbe wa Ulaya pia alikuwa na nia ya kusikiliza jinsi Waziri Sameh Shoukry anavyothamini maendeleo yaliyopatikana katika juhudi za ujenzi upya wa Ukanda wa Gaza, na jukumu lililochukuliwa na Misri kupunguza mvutano na kuvunja mzunguko wa vurugu uliopo. Pande hizo mbili zimekubaliana kuendelea na mashauriano na uratibu mnamo kipindi kijacho.