Waziri wa Mambo ya Nje afanya mazungumzo ya simu Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki
Ali Mahmoud
Balozi Ahmed Abu Zeid, Mzungumzaji rasmi wa Wizara ya Mambo ya Nje, alisema kuwa Bw. Sameh Shoukry, Waziri wa Mambo ya Nje, alifanya mazungumzo ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki “Mevlut Cavusoglu” Jumatatu, Februari 6, kutoa salamu za rambirambi kwa serikali na watu wa Uturuki kwa wahanga wa tetemeko la ardhi lililokumba Uturuki, na kufikisha matakwa ya dhati ya kupona haraka kwa waliojeruhiwa.
Mzungumzaji wa Wizara ya Mambo ya nje alieleza kuwa Waziri wa Mambo ya Nje alimwambia mwenzake wa Uturuki kuwa Misri iliamua kuelekeza misaada ya haraka kwa mshikamano na serikali ya Uturuki na watu wa kidugu wa Uturuki katika kukabiliana na athari za maafa hayo, akitaka mafanikio ya juhudi za uokoaji zinazoendelea.
Balozi Abu Zeid alihitimisha taarifa yake, akiashiria kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki alipokea simu ya Bw. Sameh Shoukry kwa kuthamini na Shukrani, akitoa Shukrani za nchi yake kwa mshikamano uliooneshwa na Misri kwa Uturuki katika msiba huo mbaya.