Dkt.Mustafa Al-feky
Mwanasiasa mmisri maarufu
Amezaliwa tarehe ya kumi na nne, mwezi wa Novemba, mwaka wa elfu moja mia tisa arubaini na nne katika kituo cha Almahmodya mkoani Albuhayra, amepatia uzamili kutoka kitivo cha uchumi na sayansi za kisiasa kutoka chuo kikuu cha Kairo katika mwaka wa elfu moja mia tisa sitini na sita, pia amepatia shahada ya daktari katika sayansi za kisiasa kutoka chuo kikuu cha London, mwaka wa elfu moja mia tisa sabini na saba.
Al-feky amejiunga uwanja wa kidiplomasia na amefanya kazi katika madaraka mengi muhimu ya kidiplomasia, ambapo amefanya kazi katika ubalozi wa Misri katika nchi mbili za Uingereza na Uhindi, pia amekuwa balozi wa Misri nchini Austria, na balozi asiyekaa katika Jamhuri ya Slovakia na Jamhuri ya Slovenia, pia amekuwa mjumbe Misri katika mashirika ya kimataifa mjini Vienna
Al-feky amefanya kazi katibu na Rais wa zamani wa Misri (Mohamed Hosny Mubarak) kwa Habari mnamo wa (1992 – 1985), pia amefundisha katika chuo kikuu cha Marekani, ambapo amesimamia idadi ya ujumbe wa kisayansi.
kwa upande wa kisiasa, Al-feky amekuwa mojawapo ya wanachama wa bunge katika baraza la watu kwa jimbo la Damanhor, na amekuwa mwakilishi wa chama cha kitaifa cha kidemokrasi, mwaka wa elfu mbili na tano, pia amekuwa mwenyekiti wa Kamati ya mahusiano ya nje katika baraza la watu mnamo wa (2010 – 2005).
Ameshinda tuzo nyingi ikiwa ni pamoja na kombe la Hotuba katika wiki ya vijana wa vyuo vikuu vya Misri, mwaka wa elfu moja mia tisa sitini na tano, na ameshinda tuzo ya kwanza katika insha ya kisiasa kwa vijana kutoka baraza kuu la kisayansi, sanaa na fasihi, mwaka wa elfu moja mia tisa sitini na sita.
Pia Al-feky amepatia tuzo ya mwandishi bora wa mawazo ya kisiasa kutoka maonyesho ya kimataifa ya Kairo kwa kitabu, na tuzo ya nchi ya kuhimiza katika mwaka wa elfu moja mia tisa tisini na nne, pamoja na Nishani ya sayansi na sanaa ya daraja la kwanza kutoka serikali ya Austria, na medali kubwa zaidi ya Austria iliyopewa kwa mabalozi wageni .
Vyeo ambavyo amevifanya kazi :
1- Mkurugenzi wa Maktaba ya Aleskandaria 11/5/2017.
2- Mwanachama wa baraza la kitaifa la haki za kibinadamu tangu mwaka (2004), na mwanachama wa Muungano wa waandishi tangu mwaka (2006), na mwanachama wa shirika la sayansi la Kimisri ambalo limejengwa mwaka (1798) tangu mwaka (2007), na mwanachama wa baraza kuu la utamaduni tangu mwaka (2007), na mwanachama wa baraza kuu la masuala ya Kiislamu na mwandishi wa Kamati ya mawazo ya Kiislamu tangu mwaka (2008), mwanachama wa baraza la kitivo cha uchumi na sayansi za kisiasa, chuo kikuu cha Cairo tangu mwaka (2008).
3- Mkuu wa chuo kikuu cha Uingereza nchini Misri ( Februari 2005 – April 2008 ).
4- Mwanachama mtendaji katika chuo cha kimataifa cha mafunzo ya kimikakati mjini London tangu mwaka (2008).
5- Mwanachama wa Kamati ya Mashariki ya Kati katika muungano wa bunge la kimataifa (2005), na mwanachama wa Kamati ya ushauri kwa muungano wa bunge la kimataifa iliyofuata umoja wa mataifa, akiwasilisha mataifa ya kiarabu peke yake (2008).
6- Mwanachama wa baraza la Misri la masuala ya nje tangu (2001),na mwanachama wa baadhi ya jumuia
husika nchini Misri.
7- Mwanachama wa baraza la watu juu ya uchaguzi wa mwaka (2005) kwa jimbo la Damanhor.
8- Balozi wa Misri kwenye jamhuri ya Asturia .
9- Balozi asiyekaa katika Jamhuri za slovakia, Slovenia na Kroatia. (1999 – 1995).
10- Mkurugenzi wa chuo cha mafunzo ya kidiplomasia (1995 – 1993).
11- Profesa wa sayansi za kisiasa katika sehemu kuu za mafunzo katika chuo kikuu cha Marekani nchini Misri kwa muda wa miaka kumi na tano (1993 – 1979).
12- Mjumbe wa kudumu kwa Misri katika mashirika ya kimataifa katika mji mkuu wa Austria (Vienna), kama vile shirika la kimataifa la nishati ya atomiki na mashirika ya umoja wa mataifa kwa muda wa miaka nne.
13- Katibu wa rais Mohamed Hosny Mubarak kwa Habari kati ya miaka miwili ya 1992 – 1985.
14- Amefundisha katika chuo kikuu cha Marekani, na amesimamia juu ya tasnifu kadhaa za kisayansi.
15- Mshauri wa ubalozi wa Misri mjini New Delhi (1983 – 1979)
16- Katibu wa pili wa ubalozi wa Misri na balozi mdogo wa Misri mjini London (mpaka mwaka 1975).
Tuzo :
1- Amepatia kombe la Hotuba katika wiki ya vijana wa vyuo vikuu vya Misri, mwaka wa (1965).
2- Amepatia tuzo ya kwanza katika insha ya kisiasa kwa vijana kutoka baraza kuu la kisayansi, sanaa na fasihi, mwaka wa (1966).
3- Amepatia tuzo ya kitabu bora zaidi katika mawazo ya kisiasa kutoka maonyesho ya kimataifa ya Cairo kwa kitabu.
4- Amepatia tuzo ya nchi ya kuhimiza, mwaka (1994).
5- Ameshinda medali ya sayansi na sanaa ya daraja la kwanza kutoka serikali ya Austria mwaka (1998).
6- Amepatia Nishani kubwa zaidi ya Austria iliyopewa kwa mabalozi wa nchi za kigeni.
7- Balozi wa Vatican, mkuu wa mabalozi nchini Austria, amempa medali kutoka papa wa Vatican.
Maandishi yake :
1- Anaandika katika magazeti mengi kama vile gazeti la Alahram, gazeti la maisha ya London na ana safu maalumu katika gazeti la Al-masri Al-yom (Mmisri leo) na ana Maandishi mengi.