Rais wa Rwanda Paul Kagame amewasili Mjini Bujumbura, Burundi kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) ulioitishwa na Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuia hiyo.
Rais Kagame anakanyaga Ardhi ya Burundi kwa mara ya kwanza tangu 2008. Mkutano huo utaangazia masuala ya usalama wa kikanda hususani mashariki mwa DRC.