Habari Tofauti

Waziri wa Afya na Ujumbe wa Umoja wa Afrika wajadili ushirikiano wa wakati ujao ili kuimarisha uwezo wa Misri katika uwanja wa uzalishaji wa chanjo na Seramu za matibabu

Mervet Sakr

Dkt. Khaled Abdel Ghaffar, Waziri wa Afya na Idadi ya Watu, alipokea ujumbe kutoka Umoja wa Afrika, kujadili njia za kuimarisha ushirikiano katika kusaidia sekta ya afya, katika Wizara ya Afya na Idadi ya Watu.

Mwanzoni mwa mkutano huo, Waziri aliukaribisha ujumbe wa Afrika wakati wa ziara yake nchini Misri, kukagua makao makuu ya Kampuni ya Holding ya Chanjo na Seramu za matibabu “VACSERA” huko Agouza na jiji la Sita ya Oktoba, ambapo ziara hiyo ilidumu kwa siku mbili kujifunza kuhusu vifaa na uwezo wa kampuni hiyo kwa uzalishaji wa chanjo na seramu za matibabu.

Dkt. Hossam Abdel Ghaffar, Msemaji wa Wizara ya Afya na Idadi ya Watu, alieleza kuwa waziri huyo alijadiliana na masuala ya ujumbe wa ushirikiano wa baadaye kati ya Misri na Umoja wa Afrika katika uzalishaji wa aina mbalimbali za chanjo na seramu za matibabu kupitia viwanda vya VACSERA, kwa lengo la kufikia utoshelevu wa ndani ndani ya nchi za Afrika.

Abdul Ghaffar alieleza kuwa Waziri huyo alifahamishwa kuhusu mpango na juhudi za Umoja wa Afrika za kuboresha viwango vya chanjo katika Bara la Afrika, na kuongeza utengenezaji wa chanjo katika Bara la Afrika ili kufikia asilimia 60 ya mahitaji ifikapo mwaka 2040.

Abdel Ghaffar ameongeza kuwa waziri huyo anathamini juhudi za Umoja wa Afrika katika kuimarisha mifumo ya afya ya umma ili kulinda usalama wa kiafya na kiuchumi wa Bara la Afrika, akisisitiza umuhimu wa kutoa msaada kwa viwanda vya ndani nchini Misri vya chanjo na seramu za matibabu dhidi ya aina mbalimbali za magonjwa, yanayoweza kuwa kituo kikuu cha kutoa mahitaji ya Bara la Afrika.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Dkt. Heba Wali, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Hodhi kwa maandalizi muhimu na chanjo “VACSERA”, na Dkt. Mohamed Hassani, Waziri Msaidizi wa Afya na Idadi ya Watu wa Mipango ya Afya ya Umma.

Back to top button