Habari
Rais Samia Suluhu akutana na Sung Shin Rais wa Kampuni ya (SSRT)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alikutana na Rais wa Kampuni ya Utengenezaji wa Mabehewa ya Sung Shin Rolling Stock Technology (SSRT) ya Nchini Korea Bw. Gye Shul Park na Ujumbe wake uliofika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 02 Febuari, 2023.
Rais wa Kampuni hiyo ameonesha nia ya kujenga Kiwanda cha kuunga Mabehewa hapa nchini, ambayo itaweza kuleta ajira kwa Watanzania, kuongeza Pato la Taifa na pia kuzinufaisha nchi jirani.