Waziri wa Afya ashiriki shughuli za sherehe ya uzinduzi wa taasisi ya “Fahem” ya msaada wa saikolojia
Dkt. Khalid Abdul Ghaffar ashuhudia utiaji saini wa itifaki ya ushirikiano kati ya Wizara ya Afya na taasisi ya “Fahem” kwa msaada wa kisaikolojia.
Dkt. Khalid Abdul Ghaffar, Waziri wa Afya na Makazi, leo Ijumaa, alishiriki katika shughuli za sherehe ya uzinduzi wa taasisi ya “Fahem” kwa msaada wa kisaikolojia, kwa mahudhurio ya mwanzilishi na mwenyekiti wa bodi ya wadhamini, Balozi Nabila Makram Abdul Shahid.
Waliohudhuria sherehe ya uzinduzi wa taasisi ya “Fahem” ni idadi ya mawaziri, mabalozi, magavana, wajumbe wa Seneti na manaibu, wakuu wa mabaraza ya kitaifa, wahusika wakuu, wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, madaktari wa tiba ya akili, waandishi na wasomi, na wawakilishi wa vyama na taasisi za jamii ya kiraia.
Dkt. Hossam Abdel Ghaffar, Msemaji rasmi wa Wizara ya Afya na Makazi, alisema kuwa Waziri wa Afya na Makazi, alishiriki katika kikao cha mazungumzo kuhusu afya ya akili nchini Misri, ambapo Waziri alipitia juhudi zilizofanywa na Wizara ya Afya na Makazi katika kutoa huduma za matibabu ya magonjwa ya akili, na jinsi ya kuepuka maambukizi kwake, akiashiria umuhimu wa ushirikiano kati ya mamlaka zote zinazohusika na washirika kukabiliana na matukio yoyote ya kisaikolojia yanayoweza kutokea katika jamii ya Misri.
“Abdel Ghaffar” aliongeza kuwa Waziri alibainisha kuwa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi alipitisha mpango unaolenga kutunza afya ya akili ya wananchi, ambapo Waziri alisisitiza kuzingatia mhimili wa utafiti wa kutoa ramani sahihi ya magonjwa nchini Misri, akibainisha tafiti zinazoonesha kuwa mtu mmoja kati ya watu wanne Duniani anapatwa na ugonjwa wa kisaikolojia, akisisitiza kuwa unyanyapaa wa jamii ni mojawapo ya matatizo maarufu yanayoikabili Misri katika uwanja wa kutibu magonjwa ya akili.
“Abdel Ghaffar” aliashiria kuwa Dkt. Khalid Abdul Ghaffar, Waziri wa Afya na Makazi, wakati wa shughuli za sherehe hiyo, alishuhudia kusainiwa kwa itifaki ya ushirikiano kati ya Wizara ya Afya na taasisi ya “Fahem” kwa msaada wa kisaikolojia, kwa lengo la kutoa huduma za matibabu ya magonjwa ya akili, kupitia kutoa madaktari hodari waliohitimu mafunzo ya kutibu wagonjwa katika mazingira salama na ya siri.
Msemaji rasmi wa Wizara ya Afya na Makazi alieleza kuwa kwa mujibu wa itifaki hiyo, uwezo wa madaktari vijana wa akili wanaofanya kazi katika hospitali za serikali unaungwa mkono kupitia ushiriki wao katika semina za kisayansi, pamoja na kuwa taasisi hiyo huvutia madaktari wa Misri wanaoishi nje ya nchi kujitolea kama wataalamu wa tiba kwenye jukwaa la kitaifa la kielekteroniki la matibabu ya afya ya akili na madawa ya kulevya katika Wizara ya Afya (https://nmhp.mohp.gov.eg/mental/web/ar).
“Abdel Ghaffar” aliendelea kuwa taasisi ya “Fahem” inashiriki katika maendeleo ya hospitali kubwa za akili, pamoja na ushiriki wa taasisi katika kusaidia maendeleo ya mageuzi ya kidijitali ya huduma za kisaikolojia, na pia taasisi hutoa msaada wa kisaikolojia kwa wale wanaohusika na kuwatunza wagonjwa wa akili.
“Abdel Ghaffar” alibainisha kuwa itifaki hiyo inalenga kuwaandaa wahitimu kutoka katika idara za saikolojia kuchukua jukumu lao katika kutoa huduma za afya ya akili, pamoja na kuwaelimisha wananchi kwa njia za kuwasiliana na watoa huduma za afya ya akili katika Wizara ya Afya, na jinsi ya kunufaika na huduma hizo.
Kwa upande wake, Balozi Nabila Makram, mwanzilishi na mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya “Fahem” kwa msaada wa kisaikolojia, alisema kuwa taasisi inalenga kuunga mkono na kusaidia watoto na vijana katika kukabiliana na shida zao za kisaikolojia na kugundua ugonjwa wao mapema, kupitia ushirikiano na sekretarieti kuu ya afya ya akili ya Wizara ya Afya na Makazi, na idadi ya madaktari wa akili waandamizi waliojiunga na bodi ya wadhamini ya taasisi.
Itifaki hiyo ilisainiwa na Dkt. Manan Abdel Maqsoud, Katibu Mkuu wa Sekretarieti Kuu ya Afya ya Akili na matibabu ya kulevya katika Wizara ya Afya na Makazi, na Balozi Nabila Makram Abdelshahid, mwanzilishi na mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya taasisi ya “Fahem” kwa msaada wa kisaikolojia.