Vijana Na Michezo

Waziri wa Vijana na Michezo akagua banda la wizara hiyo baada ya ufunguzi wa toleo la 54 la Maonesho ya Vitabu

Ashraf Sobhy: katika usanifu wetu wa banda la Wizara kwenye maonesho hayo, tulikuwa na hamu ya kutoa sura ifaayo ya utamaduni na ufahamu kwa vijana wa Misri.

Waziri wa Vijana: ushirikiano wa kimkakati unatuleta pamoja na Wizara ya Utamaduni katika ngazi zote, ambayo muhimu zaidi ni Maonesho ya Vitabu.

Waziri wa Michezo: Timu ya Vijana ya “Mimi ni Mjitolea” katika Maonesho ya Vitabu wakifanya kazi usiku na mchana kutoa msaada kwa wageni kwa msaada na imani kubwa kutoka kwa Wizara.

Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo alikagua banda la Wizara ya Vijana na Michezo kwenye Maonesho ya Vitabu, baada ya ufunguzi wa toleo la 54 la maonesho hayo, chini ya kauli mbiu isemayo: “Kwa jina la Misri: Pamoja: Twasoma… Twafikiri… Twaunda.” ambalo shughuli zake zitafanyika kuanzia 25 Januari hadi 6 Februari ijayo, kwenye Kituo cha Maonesho na Mikutano ya Kimataifa ya Misri huko The 5th Settlement.

Banda la Wizara ya Vijana na Michezo linajumuisha maonesho kadhaa, ambapo kazi za sekta mbalimbali za wizara hiyo, “Maendeleo ya watoto – Maendeleo ya Vijana – Uwezeshaji wa Vijana – Bunge na Elimu ya Kiraia – Maendeleo ya Michezo”, pia yanaoneshwa yale yanayotolewa na Jukwaa la Vijana la Taifa “Kayani” na lililozinduliwa chini ya uangalizi wa Waziri mkuu, pamoja na mapitio ya mradi wa “Rayhana” na banda la wizara hiyo kwa mara ya kwanza linapokea shughuli kadhaa za kiutamaduni na semina kupitia ajenda ya matukio iliyoandaliwa na idara zote kuu katika wizara.

Kwa upande wake, Dkt. Ashraf Sobhy alisema: “Wizara ya Vijana na Michezo daima ina uangalifu wa kukuza uelewa na ujuzi kwa vijana wa Misri kupitia kuwafanyia kazi watoto na vijana wa rika zote, na kufanya kazi ya kuwapa vijana uzoefu, kukuza uwezo wao na kuwawezesha katika nyanja za kiuchumi, ujasiriamali na ajira, na kuendeleza uaminifu na unganisho na kuwaelimisha kisiasa na kuwahimiza kushiriki katika kazi za umma, na haiwezi kupuuzwa athari za kufanya mazoezi kwenye afya zao za akili na kisaikolojia kupitia shughuli za michezo.

Kupitia ziara yake, Waziri wa Vijana na Michezo alishughulikia nafasi na ushiriki wa wajitolea wa Wizara ya Vijana na Michezo katika kuandaa matukio makubwa ya kitaifa, alisema: “kwa miaka sita wajitolea wa Wizara ya Vijana na Michezo walishiriki katika kuandaa Maonesho ya Vitabu kupitia uungaji mkono wa mpango wa Mimi ni Mjitolea, na kwa miaka hiyo sita, vijana wa Misri wamekuwa mfano wa kuigwa katika nidhamu na mfano wa kuongoza katika kuwashirikisha vijana katika sekta ya matukio kutoka nchi za eneo”.

Mwishoni mwa ziara yake kwa maonesho hayo, Waziri huyo aliishukuru Wizara ya Utamaduni kwa msaada uliotolewa nayo kupitia Mamlaka Kuu ya Vitabu ya Misri, pia kwa Kituo cha Maonesho ya Kimataifa cha Misri kwa maandalizi mazuri na ushirikiano wenye tija kwa miaka mingi kupitia banda la wizara, programu ya kujitolea na programu ya kiutamaduni.

Waziri wa Vijana na Michezo pia alikagua mabanda kadhaa ya baadhi ya nchi na mashirika yanayoshiriki katika maonesho hayo.

Waliohudhuria Ufunguzi huo ni Jihan Hanafi, Mkuu wa Utawala Mkuu wa Maendeleo ya Vijana, Hala Othman, Mkurugenzi Mkuu wa Utawala Mkuu wa Programu za Vijana wachanga, Mustafa Ezz Al-Arab, Mratibu wa Wizara ya Vijana wachanga kwa Maonesho ya Vitabu.

Back to top button