Dkt. Sewilam:
– Misri daima ipo kwa ajili ya maendeleo ya Sudan Kusini na kuunga mkono wananchi wa Sudan Kusini ndugu.
– Kina cha mahusiano ya Misri na Sudan kusini kinatusukuma kufanya kazi zaidi katika kuimarisha vifungo vya ushirikiano, upatano na uwekezaji katika nyanja mbalimbali.
– Miradi inayotekelezwa na Misri inalenga kuwahudumia wananchi kupitia kutoa maji safi ya kunywa na kupunguza hatari za mafuriko na kudumisha afya ya umma.
– Kipindi cha mwisho kilishuhudia utekelezaji wa miradi katika nyanja za umeme, afya, elimu, usafiri, mafunzo, ufadhili wa masomo, rasilimali za maji na ufunguzi wa Benki ya Taifa ya Misri jijini Juba.
– Nia ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, na kipindi kijacho kitashuhudia utekelezaji wa miradi zaidi ya maendeleo ambayo inavutia maslahi ya Serikali ya Sudan Kusini.
– Kujadili njia za kufungua njia kwa makampuni ya Misri kufanya kazi katika Jamhuri ya Sudan Kusini, haswa katika nyanja za umeme, nishati, mafuta ya petroli na miundombinu.
Katika mfumo wa ziara yake katika nchi ndugu ya Sudan Kusini.. Mheshimiwa Dkt. Riek Machar, makamu wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Sudan kusini, alimpokea Mheshimiwa Prof. Hani Sewilam, Waziri wa Rasilimali za Maji na Umwagiliaji, na ujumbe rasmi uliomuambatana na Mheshimiwa Waziri, kwa mahudhurio ya Bw. Balozi Moataz Mustafa Abdel Kader, Balozi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri kwa Sudan Kusini.
Wakati wa mkutano, Dkt. Sewilam alielezea furaha yake kukutana na Dkt. Riek Machar, akisisitiza kina cha mahusiano ya Misri na Sudan Kusini katika ngazi zote, haswa ushirikiano katika uwanja wa rasilimali za maji na umwagiliaji, unaoendelea kwa miaka mingi wakati ambao miradi mingi ya maendeleo imetekelezwa na ina faida moja kwa moja kwa wananchi wa nchi ya Sudan Kusini, na inazingatiwa mfano wa mafanikio ya ushirikiano kati ya Misri na ndugu zake wa Afrika, na kwamba kina cha mahusiano ya Misri na Sudan kusini kinatusukuma kufanya kazi zaidi katika kuimarisha ushirikiano, upatano na uwekezaji katika nyanja mbalimbali.
Dkt. Sewilam aliashiria kuwa miradi inayotekelezwa na Misri, kimsingi inalenga kuwahudumia wananchi wa nchi ya Sudan Kusini kupitia kutoa maji safi ya kunywa, kupunguza hatari za mafuriko na kudumisha afya ya umma, kipindi kilichopita pia kimeshuhudia miradi kadhaa ya ushirikiano yenye tija kati ya nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali kama vile umeme, afya, elimu, usafiri, ufunguzi wa Benki ya Taifa ya Misri huko Juba, mafunzo, ufadhili wa masomo na rasilimali za maji, pamoja na ziara za pamoja katika ngazi zote za urais na serikali.
Mheshimiwa James Wani, makamu wa Rais wa Jamhuri anayehusika na sekta ya uchumi nchini Sudan Kusini, pia alimpokea Prof. Hani Sewilam, ambapo mkutano ulishughulikia njia za kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali, na Dkt. Sewilam alisema kuwa Misri daima ipo kwa ajili ya maendeleo ya Sudan Kusini na kuwaunga mkono wananchi wa Sudan Kusini ndugu, na ina uangalifu wa kuimarisha mahusiano ya ushirikiano wa kiuchumi na nchi ya Sudan Kusini na uanzishaji wa miradi ya uwekezaji, kuhamasisha wafanyabiashara wa Misri kuchangia kuendeleza maendeleo na uchumi nchini Sudan Kusini, akisisitiza kuwa kipindi kijacho kitashuhudia utekelezaji wa miradi zaidi ya maendeleo inayovutia maslahi ya nchi ya kidugu ya Sudan Kusini.
Pia, Mheshimiwa Taban Deng, makamu wa Rais wa Jamhuri alimpokea na anayehusika na miradi na sekta ya miundombinu, Prof. Hani Sewilam, ambaye alisema kuwa mkutano huo ulishughulikia njia za kuimarisha miradi ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika uwanja wa rasilimali za maji na umwagiliaji, pamoja na kujadili njia za kufungua njia kwa makampuni ya Misri kufanya kazi katika Jamhuri ya Sudan Kusini, haswa katika nyanja za umeme, nishati, mafuta ya petroli na miundombinu.