Balozi wa Misri nchini Sudan akutana na waziri wa Mawasiliano na mabadiliko ya kidijitali
Mervet Sakr
Balozi wa Misri mjini Khartoum Hani Salah alikutana na Adel Hassan Al-Hussein, Kaimu Waziri wa Mawasiliano na Mabadiliko ya Kidijitali wa Sudan, ambapo pande hizo mbili zilipitia maendeleo yanayohusiana na mipango ya ushirikiano iliyopo kati ya Misri na Sudan katika nyanja za mawasiliano ya simu, mabadiliko ya kidijitali na posta, na kujadili njia za kusonga mbele katika kuziimarisha mnamo kipindi kijacho.
Kwa upande wake, Balozi Hani Salah alielezea matarajio ya Misri ya ushiriki wa Waziri wa Mawasiliano na Mabadiliko ya Kidijitali wa Sudan katika mikutano ya kikao cha 26 cha Baraza la Mawaziri wa Mawasiliano na Teknolojia wa Kiarabu, kilichopangwa kufanyika Januari 23 mjini Kairo, pamoja na kukutana na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Taarifa na maafisa wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ya Misri, kujadili njia za kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya nchi hizo mbili.
Waziri wa Mawasiliano na Mabadiliko ya Kidijitali wa Sudan pia alisifu ushirikiano uliopo na Misri, akielezea matarajio ya upande wa Sudan kufaidika na utaalamu wa Misri katika nyanja nyingi, hasa mabadiliko ya kidijitali, miji mahiri na nyuzi za macho.