Habari

Rais El-Sisi akagua Chuo cha Kijeshi cha Misri

Ali Mahmoud

0:00

Rais Abdel Fattah El-Sisi alitembelea Chuo cha Kijeshi cha Misri, Alfajiri siku ya Alhamisi, ambapo aliongozana na Luteni Jenerali Mohamed Zaki, Mkuu wa Majeshi, Waziri wa Ulinzi na Uzalishaji wa Kijeshi, na Luteni Jenerali Osama Askar, Mkuu wa Majenerali na idadi ya viongozi wakuu wa majeshi.

Msemaji wa Urais wa Jamhuri alisema kuwa Mheshimiwa Rais alishiriki na wanafunzi wa Chuo wakati wa utekelezaji wa shughuli na mazoezi kadhaa ambayo wanafunzi wapya wa Chuo na Vyuo vya Kijeshi hufunzwa kila siku katika makao makuu ya Chuo cha Kijeshi, ambapo shughuli hizo zilijumuisha mazoezi kadhaa ya michezo yaliyofanywa katika mstari wa mazoezi ya kimwili ya michezo mbalimbali yanayochangia kudumisha viwango vya juu vya utimamu wa mwili kwa wanafunzi, pia Mheshimiwa Rais alitazama shughuli kadhaa za mafunzo ya kijeshi kwa wanafunzi zinazofanywa kwa mujibu wa mifumo ya kisasa zaidi ya maandalizi na mazoezi yaliyoendelezwa ambayo yalionyesha jinsi wanafunzi wapya wanavyojiamini na kiwango cha juu cha nidhamu wakati wa mazoezi ya kijeshi.

Mheshimiwa Rais alikagua pia, idadi ya maeneo ya mazoezi ya wanafunzi, ikiwa ni pamoja na kupita katika bwawa la kuogelea la kielimu, viwanja vya mazoezi ya mwili vilivyoendelezwa, uwanja ulio wazi wa maandalizi ya viungo, na uwanja unaoiga vita ambapo Mheshimiwa Rais alishuhudia utekelezaji wa wanafunzi kwa zoezi la upigaji risasi kwa chombo cha uigaji wa kupiga risasi kinachohakikisha uhalisia katika utekelezaji wa zoezi, kama vile kupita viwanja vya (Al Tahady / CrossFit), sehemu kuendesha farasi na uwanja wa Al-Tahmel.

Mheshimiwa Rais alisifu alichokitazama wakati wa ziara hiyo kuhusu maandalizi ya hali ya juu ya wanafunzi hao wapya, pia aliwatakia kudumisha utayari wao wa hali ya juu wa kimwili na kiakili, na kuzingatia maadili ya juu na ya heshima ya kijeshi ambayo kwa muda mrefu yamejulikana na taasisi ya kale ya Jeshi la Misri, Mheshimiwa Rais pia alifanya mazungumzo ya wazi na wanafunzi wapya kuhusu mada na masuala kadhaa yanayotokea ndani na kikanda, akipitia juhudi zilizofanywa na serikali ya Misri katika nyanja mbalimbali waweze kutathmini hali hiyo kwa usahihi na kwa msingi wa maarifa sahihi.

Rais pia alikutana na baadhi ya familia na wazazi wa wanafunzi wapya wakati wa ziara yao kwa watoto wao, na alitoa salamu na shukrani kwao kwa juhudi zao katika kuwalea watoto wao kwa misingi na maadili yanayojikita katika uzalendo.

 

Back to top button