Wajumbe wa Muungano wa utekelezaji wa mradi wa Bwawa na Kituo cha kuzalisha Umeme wa Maji cha Julius Nyerere wakiwa katika ziara ya kukagua mradi huo
Ali Mahmoud

Ndani ya mfumo wa ufuatiliaji wa mara kwa mara wa mradi wa Bwawa na Kituo cha Umeme wa Maji cha Julius Nyerere nchini Tanzania, unaotekelezwa na muungano wa kampuni za “Makandarasi wa Kiarabu” na “Al-Sewedy Electric” Mhandisi Ahmed Al-Assar, Naibu wa kwanza wa Mwenyekiti wa kampuni ya Makandarasi wa Kiarabu, akiongozana na mhandisi Wael Hamdi, Naibu Mwenyekiti wa kampuni ya Al-Sewedy Electric, na Mhandisi Hossam El-Din Al-Rifi, mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa Makandarasi wa Kiarabu na msimamizi wa mradi huo, walifanya ziara ya ukaguzi kwa mradi huo, ulioshuhudia sherehe kubwa mnamo tarehe 22 Desemba iliyopita wakati wa ujazaji wa kwanza wa ziwa la Bwawa, kwa mahudhurio ya Mheshimiwa Mama Samia Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kwa mahudhurio ya ujumbe wa Misri uliojumuisha Balozi Sameh Shoukry, Waziri wa Mambo ya Nje, na Dkt. Assem Al-Jazzar, Waziri wa makazi, vifaa na jamii za ndani, ambaye mara kwa mara afuatilia maelezo yote ya mradi ulioagizwa na uongozi wa kisiasa, na idadi kubwa ya waheshimiwa na wawakilishi wa Wizara, Mashirika na Benki za Misri walishiriki pia katika sherehe hiyo.
Waliohudhuria ziara ya ukaguzi ni Mhandisi Ayman Attia, na Mhandisi Rafi Youssef, makamu wa Mkurugenzi wa Muungano huu, Mhandisi Darem Debsi, mwakilishi wa muungano kwa mteja, Mhandisi Osama Shawkat, Naibu Meneja wa mradi wa kazi za ujenzi, Mhandisi Mohamed Zaki, meneja wa mradi wa kazi za electromechanics, mhandisi Nada Atef, meneja wa mradi wa mabwawa madogo, na mhandisi Ahmed Al-Minshawi, meneja wa mradi wa kazi za nguvu ya umeme kwa jengo la turbine, ambapo bodi ya wakurugenzi wa Muungano ilifanya ziara ya ukaguzi kwa sekta mbalimbali za mradi huo pia ulifanyika mkutano na wasimamizi wa sekta mbalimbali za mradi huo kufuatilia maendeleo ya kazi hizo, haswa katika hatua zilizofuata ujazaji wa kwanza wa Ziwa la Bwawa hilo, na ilisisitizwa kuwa lazima kuendelea kuwajibika kwa viwango vya juu zaidi vya utekelezaji na viwango vya ubora vinavyohitajika.