Habari

Rais El-Sisi afuatilia juhudi za kuendeleza mfumo wa elimu ya msingi katika nyanja zake mbalimbali

Ali Mahmoud

Rais Abdel Fattah al-Sisi amekutana leo, na Dkt. Mustafa Madbouly, Waziri mkuu, Dkt. Mohamed Mait, Waziri wa Fedha, na Dkt. Reda Hegazi, Waziri wa Elimu na Elimu ya Ufundi.

Mzungumzaji rasmi wa Urais wa Jamhuri alisema kuwa mkutano huo ulishughulikia ufuatiliaji wa ” Juhudi za kuendeleza mfumo wa elimu nchini Misri katika hatua zake mbalimbali za kimsingi.”

Katika muktadha huu, Mheshimiwa Rais alielekeza kuzingatia kuendeleza kada za binadamu na mfumo wa walimu, na kupanua uanzishaji wa shule mashuhuri mpya za kila aina, ndani ya mfumo wa mwelekeo wa kimkakati na wa thabiti wa serikali kwa kusaidia uwekezaji katika elimu kwa ajili ya kuchangia kujenga utu wa Misri tangu utoto katika kipindi cha awali ya Chuo Kikuu, kwa lengo la kuboresha vizazi vipya kisayansi, kiutamaduni na maarifa.

Pia Rais alielekeza kuimarisha shughuli za Wizara ya Elimu kuhusu upanuzi wa shule za teknolojia za matumizi na kueneza ufahamu wa jamii juu ya umuhimu wao, kama kielelezo cha mafanikio kwa shule maalumu zinazotegemea ushirikiano na sekta binafsi kukidhi mahitaji yake ya kada maalumu za kiufundi, haswa katika uwanja wa mawasiliano na teknolojia ya habari unaowakilisha moja ya mambo muhimu ya mchakato wa viwanda na maendeleo, pamoja na kazi za ufundi.

Mzungumzaji rasmi huyo alieleza kuwa Dkt. Reda Hegazi alipitia mipango ya Wizara ya Elimu kuhusu uboreshaji kamili wa mfumo wa elimu ya msingi nchini Misri na vipengele vyake mbalimbali, haswa msaada wa kada za binadamu za walimu, utoaji wa idadi inayofaa kutoka kwao kulingana na idadi ya wanafunzi, pamoja na kuwazoeza na kuwawezesha wakuu wa shule, pamoja na kuendeleza mitaala katika hatua mbalimbali za masomo.

Waziri wa Elimu pia alionesha mpango wa Wizara wa kuendeleza mfumo wa shule na kuanzisha shule mpya katika ngazi ya Jamhuri, haswa mfululizo wa shule za “Misri bora” zinazofanya kazi kwa mfumo wa siku nzima, pamoja na “Shule Rasmi za Kimataifa IPS” na idadi yake ni 20 katika ngazi ya mikoa, kama vile shule za Nile na mipango ya Wizara kutangaza cheti chake ndani na nje katika uratibu na mashirika ya kitaaluma ya kimataifa maalumu katika kutoa vibali vinavyohusiana, ambayo itafanya jukumu lake la kutoa mazoezi kwa walimu na wale wanaosimamia mchakato wa elimu katika shule hizi, pamoja na shule za Misri-Kijapani na kuanzisha zaidi yao kulingana na viwango vya kibali vya kijapani, ambavyo vinategemea kutoa Elimu Jumuishi “Takatsu”, pamoja na kupanua uanzishaji wa Shule za Teknolojia ya kutumika kuchangia utoaji wa elimu ya kiufundi ya hali ya juu iliyoendelezwa kukidhi mahitaji ya viwanda na maendeleo, kwa ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi, katika kusaidia juhudi za serikali kwa njia ambayo inaunga mkono juhudi za serikali za kufikia uwekezaji bora wa utajiri wa binadamu ambao Misri inajaa, pia kuufungua nyanja za kazi za kigeni kwa wahitimu wanaojulikana kutoka shule hizo.

Rais pia alielezwa juhudi za Wizara ya Elimu ya kuanzisha, kuendeleza na kuongeza ufanisi wa majengo ya elimu katika ngazi ya Jamhuri, kwa uratibu na kurugenzi mbalimbali za elimu, kama vile mpango wa “Maisha Bora” kuendeleza vijiji vya mashambani mwa Misri, ambapo aliagiza Wizara ya elimu kufanya mapitio ya mara kwa mara ya vifaa na majengo ya elimu katika ngazi ya Jamhuri, kwa uratibu na sekta ya serikali za mitaa katika mikoa.

Back to top button