Habari Tofauti

Maprofesa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Marekani jijini Kairo na Chuo Kikuu cha George Washington watembelea Msikiti wa Al-Azhar

Ali Mahmoud

 Msikiti wa Al-Azhar ulipokea ujumbe kutoka Chuo Kikuu cha George Washington na Chuo Kikuu cha Marekani huko Kairo, unaojumuisha idadi ya maprofesa na wanafunzi kutoka Vyuo Vikuu vyote viwili kando ya ziara ya ujumbe wa Chuo Kikuu cha George Washington kwenda Misri katika mfumo wa kubadilishana kisayansi na kiutamaduni kati ya Vyuo Vikuu vya Misri na kigeni.

Ujumbe wa wanafunzi ulipokelewa na Dkt. Ahmed Hammam, mkurugenzi wa Idara ya masuala ya kidini kwenye Msikiti wa Al-Azhar Al-Sharif, na Sheikh Ahmed Abdul Azim Al-Tabakh, mjumbe wa ofisi ya kiufundi kwenye Msikiti wa Al-Azhar, na maafisa wa mahusiano ya umma.

Wakati wa ziara yao ya kutembelea Msikiti wa Al-Azhar, ujumbe ulisikiliza maelezo ya kina kuhusu historia ya kale ya Msikiti wa Al-Azhar, na pia, Dkt. Hammam alionesha shughuli za kisayansi na kiutamaduni maarufu zaidi zilizofanywa na Riwaq Al-Azhar ikiwa ni pamoja na semina za kuhifadhi Quran Tukufu, mihadhara ya kueleza vitabu vya urithi, mihadhara ya Riwaq ya Sayansi za Sharia na kiarabu, pamoja na Mikutano na vikao vya kisayansi na halmashauri zilizofanyika katika Msikiti wa Al-Azhar mara kwa mara.

Mwishoni mwa ziara hiyo, ujumbe huo ulionesha furaha yake kubwa ya kutembelea jengo hili adhimu, ambalo linazingatiwa Chuo Kikuu kongwe cha pili Duniani kote.

Back to top button