Habari

Balozi wa Misri mjini Lusaka azungumzia kuimarisha ushirikiano wa kimatibabu na Waziri wa Afya wa Zambia

Ali Mahmoud

Balozi wa Misri mjini Lusaka, Moataz Anwer, Jumatano, alikutana na Waziri wa Afya wa Zambia, Sylvia Masebo, katika makao makuu ya Wizara ya Afya mjini Lusaka, na hiyo katika mfumo wa maandalizi ya kuandaa ziara ya ujumbe kutoka Wizara ya Afya ya Zambia Jijini Kairo kujadili njia za kuimarisha ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika uwanja wa afya.

Balozi Moataz Anwar amesisitiza uangalifu wa Misri kuimarisha mifumo ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali zinazohusiana na sekta ya afya.

Alielezea matarajio ya upande wa Misri kupanua nyanja za ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika uwanja wa Afya, kwa kuzingatia mipango mbalimbali ya mazoezi na maendeleo ambayo inaweza kutolewa na Wizara ya Afya ya Misri na Shirika la Misri la ushirikiano kwa ajili ya maendeleo.

Kwa upande wake, Waziri wa Afya wa Zambia alikaribisha ziara hiyo, akielezea nia ya nchi yake kuimarisha mifumo ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika uwanja wa Afya ijumuishe mipango ya mazoezi, viwanda vya dawa na kubadilishana ziara na uzoefu kati ya timu za matibabu.

Back to top button