“Rais Abdel Fattah El-Sisi afuatilia maendeleo ya Mfumo wa mauzo ya nje ya kilimo wa Misri”
Ali Mahmoud
Jana, Rais Abdel Fattah El-Sisi alikutana na Dkt. Mustafa Madbouly, Waziri mkuu, Bw. Al-Sayed Al-Quseir, Waziri wa Kilimo na kufufua ardhi, na Meja Jenerali Walid Abu El-Magd, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Miradi ya Huduma ya Taifa ya Vikosi vya Wanajeshi, na Kanali Rubani Bahaa El-Ghannam, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mustakabali ya Misri kwa Maendeleo Endelevu.
Mzungumzaji Rasmi wa Urais wa Jamhuri alisema kuwa mkutano huo ulishughulikia “kufuatilia maendeleo ya Mfumo wa mauzo ya nje ya kilimo ya Misri”.
Katika muktadha huu, Waziri wa Kilimo alionesha maendeleo ya kipekee yaliyoshuhudiwa na mfumo wa mauzo ya nje ya kilimo ya Misri, haswa utawala wa taratibu za uuzaji nje na mfumo mpya wa usimbaji unaotumika sasa kwa mauzo ya nje ya kilimo ya Misri kuhakikisha ufuatiliaji wa bidhaa zinazouzwa nje na kuimarisha udhibiti wao kutoka mashamba ya kuuza nje kwenda nchi zinazoagiza, chini ya usimamizi kamili wa mamlaka ya udhibiti, na kuwapa wakulima na wauzaji nje mwongozo wote wa kiufundi unaohusu mahitaji ya mazoea mazuri ya kilimo kulingana na viwango vya juu vya uuzaji wa mazingira vinavyotumika kimataifa, na matumizi ya miche bora kwa aina zinazohitajika ulimwenguni wakati wa kutoa huduma muhimu za maabara kuhakikisha usalama wao, nalo ambalo lilionekana katika kuongezeka kwa kiasi cha mauzo ya Nje ya Misri ya mazao ya kilimo na ufunguzi wa masoko mapya ya nje, ambapo kiasi cha mauzo ya nje wakati wa 2022 yalifikia karibu tani milioni 6,43 kwa karibu nchi 160 Duniani kote kufikia mapato ya mauzo ya nje karibu dola bilioni 3,3.
Mheshimiwa Rais alielekeza uzingatiaji mkali kwa masharti ya udhibiti wa mauzo ya nje ya kilimo ya Misri kuzalisha mazao ya uuzaji nje yenye ubora unaotambulika, na utegemezi wa kipekee kwa vyombo vinavyohusishwa na mfumo wa usambaji na karantini ya kilimo, na kukabiliana na ukiukaji wowote katika muktadha huu, pamoja na kutumia viwango vya nchi zinazoagiza kwa mazao yote ya kilimo ya Misri.
Mzungumzaji Rasmi aliongeza kuwa mkutano huo pia ulishuhudia uwasilishaji wa msimamo wa juhudi za maendeleo ya mifugo, kupitia mpango wa kitaifa wa ugawaji wa maelfu ya mifugo yenye tija kwa wakulima na wafugaji wadogo, kwa lengo la kuboresha hali zao na kuwasaidia kiuchumi, na kwa uratibu kati ya Wizara husika, Shirika la miradi ya huduma ya kitaifa, sekta ya benki na mashirika jamii ya kiraia.
Katika muktadha huo, Rais alielekeza kufuatilia hali za wakulima na wafugaji wadogo mara kwa mara na kuwaunga mkono kwa kutoa msaada wa kiufundi na huduma iliyohitajika kwa mifugo, na kuongeza jukumu la ushauri la walengwa wote wa mpango wa kitaifa wa ugawaji wa mifugo.