Misri yathibitisha mshikamano wake na uungaji mkono wake kwa serikali ya Pakistan na watu wake kutokana na mafuriko yaliyoshuhudiwa
Ali Mahmoud

Balozi Dkt. Ahmed Ehab Gamal El-din, mwakilishi wa kudumu wa Misri kwenye Umoja wa Mataifa huko Geneva, alitoa taarifa ya Misri kupitia “Mkutano wa Kimataifa kuhusu uvumilivu wa hali ya hewa: Pakistan” uliofanyika leo huko Geneva.
Taarifa hiyo imesisitiza mshikamano wa Misri na uungaji mkono wake kwa serikali ya Pakistan na watu wake kwa sababu ya mafuriko ambayo nchi hiyo iliyashuhudia mnamo Mwaka uliopita na yalisababisha hasara na uharibifu mkubwa.
Taarifa hiyo pia iliashiria mawasiliano ya simu yaliyotolewa na Rais Abdel Fattah El-Sisi na Waziri mkuu wa Pakistan, Shahbaz Sharif, ambapo alitangaza utoaji wa misaada ya kibinadamu kuchangia kupunguza athari za msiba kwa watu wa Pakistan.
Taarifa hiyo pia ilionesha mafanikio yaliyofikiwa wakati wa Mkutano wa Mataifa Wanachama katika makubaliano ya mfumo ya Umoja wa Mataifa ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa COP27, chini ya Urais wa Misri, haswa uanzishwaji wa mfuko wa ufadhili wa hasara na uharibifu, uanzishaji wa mtandao wa Santiago kuhusu hasara na uharibifu na uzinduzi wa ajenda ya Sharm El-Sheikh kwa kukabiliana, nayo ni Matokeo yanayohusiana sana na yaliyoshughulikiwa mnamo mkutano wa uvumilivu wa hali ya hewa: Pakistan.
Taarifa hiyo imekaribisha ahadi zilizotolewa na nchi na taasisi za kimataifa, pamoja na kuelezea matarajio ya Misri kutoa msaada zaidi kwa Pakistan, ambayo ni moja ya nchi zinazochangia kwa kiasi kidogo katika mabadiliko ya hali ya hewa na kuathiriwa zaidi na mabadiliko hayo.
Taarifa hiyo pia imesisitiza haja ya mapitio ya muundo wa Fedha wa kimataifa ili kuhakikisha uwiano wake na malengo ya hali ya hewa, pamoja na kuharakisha mpito kutoka kwa ahadi hadi utekelezaji kusaidia watu wa Pakistan katika mgogoro huu, na kuchangia mchakato wa kujenga upya kwa kuzingatia mambo ya kukabiliana na ustahimilivu na mabadiliko ya hali ya hewa.