Miaka 63 tangu kuweka jiwe la msingi la mradi wa Bwawa la Juu, mradi mkubwa zaidi wa uhandisi mnamo karne ya ishirini
Ali Mahmoud

Dkt. Sweilem:
– Bwawa la Juu limeilinda Misri kutokana na ukame na mafuriko kwa miongo kadhaa.
– Mradi huu huwakilisha uwezo wa watu wa Misri kujenga na kufanya kazi kwa azimio na msisitizo.
– Natoa Salamu na Shukrani kwa wale wote walioshiriki katika utenzi huu wa kihistoria.
– Watu waliofanya kazi katika mradi huu wameandika historia kubwa itakayosimuliwa kwa vizazi wengi wajao.
– Kudhibiti asili ya miamba kusini mwa Misri kwa ajili ya ujenzi wa Bwawa Kubwa kama ishara maarufu na itakayodumu katika historia ya Misri.
Misri inaadhimisha leo kumbukumbu ya miaka 63 ya kuweka jiwe la msingi la Bwawa la Juu na Marehemu Rais Gamal Abdel Nasser na hiyo katika Januari 9, 1960.
Mheshimiwa Prof. Hani Sweilem, Waziri wa Rasilimali za Maji na Umwagiliaji, alisema kuwa mradi huu mkubwa unazingatiwa “mradi mkubwa zaidi wa uhandisi katika karne ya ishirini”, na mradi huu umeilinda Misri kutokana na ukame na mafuriko kwa miongo kadhaa, na unawakilisha uwezo wa watu wa Misri kujenga na kufanya kazi wakati mikono ya watu wa Misri iliweza kujenga kazi hii kubwa kwa msisitizo na azimio.
Aliongeza kuwa pia tutasherehekea mnamo siku chache, maadhimisho ya kufunguliwa kwa mradi wa Bwawa la Juu na Rais wa marehemu Mohamed Anwer Al-Sadat mnamo tarehe 15 Januari 1971, siku hii ambayo ikawa siku ya kitaifa kwa Mkoa wa Aswan.
Prof. Sweilem alitoa Salamu na Shukrani kwa wale wote walioshiriki katika kuhakikisha utenzi huu wa kihistoria wakati wafanyakazi wa mradi huu wameandika historia kubwa kusimuliwa kwa vizazi wengi wajao, wakati waliweza kudhibiti asili ya miamba kusini mwa Misri kujenga Bwawa la Juu kama ishara maarufu na itakayodumu katika historia ya Misri.
Inatajwa kwamba uamuzi wa kujenga Bwawa la Juu ulichukuliwa mnamo Mwaka1953 kwa kuunda kamati ya kuendeleza kubuni kwa mradi huo, na muundo wa Bwawa la Juu ulitengenezwa katika Mwaka 1954 chini ya usimamizi wa Mhandisi/ Moussa Arafa na Dkt. Hassan Zaki kwa msaada wa idadi ya makampuni ya kimataifa yanayohusika, Misri imeamua, wakati huo, kutaifisha Mfereji wa Suez mnamo Mwaka 1956 kutoa rasilimali za kifedha zilizohitajika kwa ajili ya ujenzi wa Bwawa la Juu, ili makubaliano ya ujenzi wa Bwawa la Juu yasainiwe mnamo Mwaka 1958 na kuweka jiwe la msingi katika Mwaka 1960.