Utamduni

“Safari za Qamar Barani Afrika” zawavutia watoto kwenye banda la Al-Azhar kwenye Maonesho ya Kitabu ya Kairo

Wao walikusanywa na Mto Nile.. Wageni watoto wa banda la Al-Azhar wachunguza Afrika na mtoto wa kike “Qamar”

Banda la Al-Azhar Al-Shareif kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kitabu jijini Kairo, kwa wageni wake kutoka kwa watoto, latoa kitabu cha “safari za Qamar Barani Afrika”, kilichoandikwa na Ibrahim Hefny na kuchorwa na Ibrahim Amr, kutoka kwa machapisho ya Jarida la watoto la Noor, lililotolewa na Shirika la Kimataifa la Wahitimu wa Al-Azhar, kinashughulikia umuhimu wa Mto Nile kwa nchi za Bara la Afrika, na jinsi ya kufaidika nao kuudumisha.

Kitabu hiki kinajumuisha hadithi 10 za kufurahisha, zinazojumuisha safari ya mtoto “Qamar”, kwa nchi za Bonde la Nile (Eritrea – Uganda – Ethiopia – Sudan – Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo – Burundi – Tanzania -Rwanda – Kenya – Misri).

Hadithi inahusu safari ya Qamar wakati yeye anatembelea Mto Nile na familia yake, kupitia meli kubwa, na wakati wa safari yeye anamuuliza baba yake maswali mengi kuhusu Afrika na Mto Nile, ili “Qamar” achunguze na kujifunza mengi kuhusu hazina na mandhari za Bara la Afrika.

Katika safari hii na “Qamar” Barani Afrika, watoto watatambua habari kuhusu Mto Nile, maana ya majina ya nchi za Bonde la Nile, mandhari maarufu zaidi katika Afrika, kutambua lugha zinazozungumzwa na Bara la Afrika, majina ya sarafu halisi zinazotumiwa na nchi za Bonde la Nile, sahani maarufu zaidi, vyakula na desturi za kijamii katika kila nchi ya Bonde la Nile.

Kitabu hicho pia kinaonesha safari ya “Qamar” kwenye milima ya Burundi, visiwa vya Nile Nyeupe na Bluu, na majasirio mengi ambayo “Qamar” ameyafanya na marafiki zake kutoka nchi 10, aliwatambua kupitia safari yake ya kufurahisha ndani ya Afrika.

Kitabu hiki kuhusu Afrika na Mto Nile kinatokana na imani ya Al-Azhar Al-Shareif kwa umuhimu wa kuwasiliana na watoto kwa lugha nyepesi inayochangia malezi yao juu ya maadili ya udugu na amani kati ya wanadamu, kuwaelimisha maadili matukufu ya kibinadamu, na kusafisha akili zao kutoka kwa mawazo yenye misimamo mikali.

Al-Azhar Al-Shareif inashiriki, kwa Mwaka wa saba mfululizo, katika banda maalum katika Maonesho ya Kimataifa ya Kitabu ya Kairo katika toleo lake la 54 kulingana na jukumu la elimu na utetezi wa Al-Azhar katika kueneza mawazo ya Kiislamu ya wastani ambalo limepitisha kwa zaidi ya miaka elfu moja.

Banda la Al-Azhar kwenye Maonesho hayo lipo katika Ukumbi wa Urithi Na. “4”, na linaenea zaidi ya eneo la mita elfu moja, linajumuisha kona kadhaa, kama vile ukumbi wa semina, kona ya fatwa, kona ya hati ya kiarabu, pamoja na kona ya watoto na maandishi.

Back to top button