Habari
WAZIRI MKUU AZINDUA RIPOTI YA UTAFITI VIASHIRIA VYA UKIMWI
0:00
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua ripoti ya utafiti wa viashiria vya UKIMWI ambayo inaonesha maambukizi mapya miongoni mwa watu wazima wenye umri zaidi ya miaka 15 yanaendelea kupungua.
“Maambukizi mapya miongoni mwa watu wazima wenye zaidi ya miaka 15 yanaendelea kupungua kutoka watu 72,000 waliokuwepo mwaka 2016/2017 hadi watu 60,000 kwa mwaka 2022/2023. Hii ni sawa upungufu wa asilimia 0.18 ambapo asilimia 0.24 ni wanawake na asilimia 0.11 ni wanaume,” amesema.
Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Desemba mosi, 2023) wakati akizungumza na mamia ya wananchi waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya sekondari ya Morogoro, mjini Morogoro.