Siasa

Rais Samia Hassan akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Brazil

Ahmed Hassan

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Brazil hapa nchini Mhe. Gustavo Martins Nogueira mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 27 Februari, 2023.

Pia rais Samia Suluhu Hassan amefanya mazungumzo na Balozi wa Brazil hapa nchini Mhe. Gustavo Martins Nogueira mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho, Ikulu Chamwino Mkoani.

Katika mazungumzo yao walisisitiza masuala ya Afya ya Mama na mtoto, maradhi ya Seli Mundu (Sickle cell) pamoja na kuendelezwa kwa ushirikiano kwenye Sekta ya Kilimo.

Back to top button