Miji Ya Misri

Sharm El-Sheikh.. Mji wa Amani

Mahali pa kukutana kwa  Ghuba mbili za Aqaba na Suez, ambapo pwani ya Bahari Nyekundu iko , na baina ya kundi la kipekee la pomboo ambalo lina sifa yake, na kati ya koloni za miamba ya matumbawe ambazo hupamba chini yake,uko mji wa Sharm El-Sheikh, ni moja wapo ya miji mizuri zaidi ulimwenguni, na moja ya vituo muhimu vya kimataifa vya kupiga mbizi ambavyo vinavutia wapendaji na wataalamu wa kupiga mbizi.

Katika eneo linalokadiriwa kama  kilomita 480, linajumuisha vituo vingi vya watalii, uwanja wa ndege wa kimataifa na kumbi nyingi za mikutano zinazohimiza kazi za pamoja baina ya nchi za ulimwengu kuhakikisha amani na maendeleo, kwa hivyo inajulikana kama Jiji la Amani. Inatembelewa na wageni kutoka kote ulimwenguni, na historia ya jiji hilo inarudi nyuma maelfu ya miaka, wakati ilikaliwa na Bedouins, lakini kuanzishwa kwake kulikuja rasmi mnamo 1968 .

Tangu tarehe hiyo, jiji hilo limeendelea kwa kasi hadi likawa mojawapo ya majiji mashuhuri ya kitalii huko Sinai na ulimwenguni, na linachukuliwa kuwa moja ya majiji manne mazuri zaidi ulimwenguni, kulingana na uainishaji wa BBC wa mwaka wa 2005. Na pia Mabadiliko ya jiji hilo kuwa mifumo ya kisasa katika usanifu, burudani, usalama na huduma za hoteli yaliliandaa kushinda Tuzo ya UNESCO na kuchaguliwa kwake miongoni mwa miji mitano bora ya amani kati ya miji 400 ya kimataifa.

Miongoni mwa maeneo muhimu zaidi ya kiutalii:

Ghuba ya Ne’ema 

Ghuba ya mchanga inayoitwa moyo wa Sharm el-Sheikh iko kwenye mahali pa kukutana kwa mabara mawili ya Asia na Afrika, na ni moja ya vivutio maarufu vya watalii katika jiji hilo, kwani inajumuisha idadi kubwa ya hoteli za kifahari na  kubwa zaidi na maeneo ya watalii, pamoja na mikahawa na migahawa ambayo hutoa vyakula vitamu zaidi maarufu na vya kimataifa.

Ghuba ya Ne’ema pia ina sifa ya pwani zake za kupendeza.Kama pwani  maarufu ya Mangharuf, ilio na maji safi, na asili ya miamba inayozunguka pwani kutoka pande fulani, eneo hilo pia ni maarufu kwa kupiga mbizi ili kuchunguza samaki warembo zaidi na miamba ya matumbawe katika Bahari Nyekundu.

Unaweza pia kufanya mazoezi ya kila aina ya shughuli za pwani na maji, Ikiwa ni pamoja na mchezo wa kuendesha boti za kioo, kayaking, kutumia parachute na kupanda mawimbi na kila aina ya shughuli za baharini, muhimu zaidi ambayo, bila shaka, ni kuogelea na kulala chini ya jua.

Na jambo  linalotofautisha Ghuba ya Ne’ema pia,ni maisha ya usiku, ambayo hukupa kile unachotafuta, iwe kwa kukaa na kupumzika ufukweni, au kukaa katika mikahawa tofauti , ambayo hutofautishwa na mapambo yao ambayo ni ya mtindo wa maisha ya Bedouin huko Sinai.

Hifadhi ya Ras Mohammed

Hifadhi ya asili ya pili muhimu zaidi Duniani, mnamo kipindi cha miaka thelathini iliyopita, baada ya Uluru-Kata Park Tjuta huko Australia, ni mfano kamili wa mfumo wa ikolojia unaojumuisha bahari na maji yake yenye kiwango cha buluu, milima na miamba inayoshuhudia asili ya Misri, mimea kama vile mikoko na shura, na halijoto ya wastani , na hewa safi, ili kujumuisha kwa ajili yetu mchoro wa asili katika maelewano ya kipekee kote ulimwenguni.

Imepakana kutoka kaskazini tambarare ya pwani ya kusini ya uwanda wa Tabba, na safu yake inaenea ndani ya Bahari Nyekundu kwa karibu kilomita 10-15. Ukingo wake wa mashariki unawakilisha ukuta wa mawe na maji ya Ghuba.

Eneo lake ni takriban kilomita za mraba 200, kati ya hizo takriban kilomita za mraba 75 ziko katika sehemu ya nchi kavu na takriban kilomita za mraba 125 ziko katika sehemu ya bahari. Ina mfereji wa mangharuf unaotenganisha Kisiwa cha Ras Muhammad na Kisiwa cha Al-Bairah,na Ziwa la uchawi na Mwamba wa Simba.

Mimea ya baharini ndani ya hifadhi inawakilishwa na mwani, ambao huchukuliwa kama kusambaza maji na oksijeni muhimu kwa njia ya usanisinuru(muundo wa nuru), kama vile nyasi, ambayo kasa na viumbe vya baharini hulisha.Kama vile nyasi, ambayo kasa na viumbe vya baharini hula, na pia inachukuliwa kuwa kitalu cha samaki wadogo ili kuwalinda dhidi ya samaki wakubwa, pamoja na miti ya mikoko, ambayo huvumilia chumvi ya bahari, kuchuja maji ya chumvi, na kuweka chumvi kwenye nyuso za majani yake.

Kuhusu wanyama wa baharini ni pamoja na moluska, mamalia, nyota ya baharini, viwavi wa baharini, miamba ya matumbawe, pomboo, kobe wa baharini na papa, pamoja na samaki ambao wana jukumu muhimu katika kuleta usawa wa mazingira kwa sababu hula mabuu ya nyota ya baharini, ambayo nayo hulisha kwenye miamba ya matumbawe, hivyo kulinda miamba hii.

Hifadhi hiyo inajumuisha fukwe zaidi ya 12, na ni kivutio cha wapiga mbizi Duniani, kwani inachanganya mazingira matatu katika mpangilio  ajabu wa mwani wa baharini, miamba ya matumbawe na samaki (samaki wa Picasso wa rangi angavu).

Chemchemi cha Mangharuf

Ni vichaka ambavyo hubadilika kulingana na kiwango cha chumvi na joto, na hutofautiana katika anatomy yake, kwani hufanya mchakato wa usanisinuru na uondoaji wa chumvi ya maji kwa wakati mmoja, na shina ni msingi wa  usanisinuru na mizizi ndani. pamoja na jukumu lake katika kunyonya maji, kwani ni njia ya kupumua, na mikoko huondoa chumvi inayopatikana ndani ya maji kwa kuitupa kwenye nyuso za majani yake, wakati mmea huu unachukuliwa kuwa mazingira jumuishi, kitalu na mahali pa kupumzika. kwa ndege wanaohama.

Mpasuko wa tetemeko la ardhi
Ni mpasuko katika ganda la ardhi , na maji hutiririka ndani yake, na uduvi wa rangi nyekundu vipofu huzaliana/huongezeka ndani yake, wenye urefu wa mita 42 na kina cha mita 14, na  imejaa viumbe kama vile mwani, ambao hawapatikani katika Bahari Nyekundu.na pia  kushikamana na bahari kupitia mabomba .

“Ziwa Elmashura ” (ziwa la uchawi) ambalo rangi zake hubadilika kuwa zaidi ya rangi moja siku nzima kulingana na nguvu na pembe ya mwanga wa jua. Mtu yeyote anayetafuta uponyaji na faraja ya kisaikolojia hukimbilia kwa sababu lina kiasi kikubwa cha madini ambayo hutumiwa kutibu   Magonjwa ya Rheumatic.

Ni “Ziwa la matakwa ” ambalo jina lake ni maarufu zaidi kati ya Wabedui, ambao huogelea humo kwa saa nyingi na kisha kurusha mawe huku wakisema matakwa yao, wakiwa na uhakika kwamba yatatimia.

 Ras Nasrani 

Eneo lenye viumbe vingi vya baharini, kutokana na utofauti mkubwa wa mandhari ya chini ya maji. Wapiga-mbizi  hupenda eneo hili kwa kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba wanaweza kuona Samaki wa shetani ya Bahari na papa wa nyangumi.

Ras om El-Said 

Eneo hilo liko kwenye ncha ya rasi ndogo,ni  umbali wa kilomita chache kutoka Ghuba ya Ne’ema,inaonesha mandhari ya ajabu ya Bahari Nyekundu na miamba ya matumbawe, na ni tulivu zaidi kuliko soko la zamani la Sharm el-Sheikh na Hifadhi ya Taifa ya Ras Mohammed, ambapo wapiga mbizi huenda kushangazwa na maumbo ya ajabu ya matumbawe, haswa miamba ya matumbawe, pamoja na wingi wa viumbe vya majini, ikiwa ni pamoja na aina mbalimbali za samaki adimu.

Hifadhi ya Nabq 

Iko kilomita 35 kaskazini mwa Sharm El-Sheikh, kati yake na Dahab na Wadi Umm Adawi katika Sinai Kusini.Mazingira yake yanatofautiana baina ya mazingira ya milima na mazingira ya jangwa,Inajumuisha kundi muhimu la wanyama na ndege, maarufu zaidi ambao ni ,pimbi, mbweha, swala, aina fulani za panya na wanyama watambaao, na ndege wengi wanaoishi na wanaohama, ambao muhimu zaidi ni korongo,furukombe,El-khawada , Mbali na aina 134 za mimea, ambapo takriban spishi 86 zimetoweka kabisa katika maeneo mengine, ikiwa ni pamoja na mmea wa mikoko unaojulikana kama mmea wa Shura ambao huishi kwenye maji yenye chumvi , kunyonya maji safi na kuondoa chumvi kwenye majani yake na kusaidia kuhifadhi mashapo, Urefu wake hauzidi mita tano, na misitu ya mikoko inachukuliwa kuwa maeneo muhimu ya kuzaliana kwa samaki na wanyama wasio na uti wa mgongo na makazi ya aina nyingi za ndege wanaohama na wakaaji.Mwaka 1992 , eneo hilo lilitangazwa kuwa hifadhi ya asili.

Mlango-Bahari wa Tiran

  Ni eneo la miamba ya  Jackson, kutokana na mikondo mikali na virutubisho vingi, miamba ya matumbawe hapa hukua kwa ajabu, ikivutia idadi kubwa na aina mbalimbali za samaki kama vile papa wa Nyundo na papa wa kijivu.

Meli ya Thistlegorm

  Ni meli iliyozama mwaka 1941, baada ya kuishambulia ilipokuwa njiani kutoka Glasgow kuelekea Alexandria, na yaliyomo ndani ya meli hiyo, ambayo ni pamoja na pikipiki, malori na magari ya kivita, yalitua kwenye sakafu ya bahari pamoja na mabaki yenyewe na shimo lililotengenezwa na bomu la Ujerumani.

Hifadhi ya Abugalum

  Iko kwenye Ghuba ya Aqaba, kwenye barabara baina ya mji wa Sharm El-Sheikh na Taba, katika eneo linaloitwa Wadi Rasasah.Ina sifa ya asili yake ya kupendeza, ambayo inakutenga kabisa na ulimwengu.

Hifadhi hiyo inachukuliwa kuwa kimbilio la wapenzi wa kupiga kambi, kwa kuwa kuna nyumba zilizojengwa kwa wicker na msitu, na hukupa vyakula maarufu vya Bedouin kama vile mkate wa kahawia, maandazi na jibini, pamoja na kunywa chai asili ya Bedouin.

Hali ya maji katika hifadhi pia ni ya kupendeza sana, kwani ina sifa ya kuwepo kwa idadi kubwa ya samaki adimu, pamoja na asili ya miamba na mapango chini ya maji.

Makumbusho ya Sharm El Sheikh

Makumbusho ya Sharm El-Sheikh ni makumbusho ya kwanza ya mambo ya kale ya Misri huko Sharm El-Sheikh, ambayo ni maarufu Duniani kwa utalii wa pwani, kuwa kitovu cha mng’ao wa kitamaduni na ustaarabu na mahali pa kukutana kwa ustaarabu wa binadamu, na nyongeza dhahiri kwa utalii unaotarajiwa katika jiji hilo, sambamba na mpango wa Wizara wa kuunganisha utalii wa burudani na utalii wa kiutamaduni, ili wageni na watalii waweze kufurahia fukwe za kupendeza na shughuli za kuvutia za baharini na ardhi katika jiji hilo, na wakati huo huo kujua ustaarabu wa kale wa Misri.

Wazo la kuanzisha  jumba la makumbusho lilianzia 1999, na iko kwenye eneo la mita za mraba 191,000. Kazi ya mradi huo ilianza mnamo 2003, kisha ikasimamishwa mnamo 2011, na kuanzishwa tena mnamo 2018 . kwa gharama ya pauni milioni 812. Makumbusho inajumuisha kumbi tatu za maonyesho, pamoja na Kwa eneo la burudani ambalo linajumuisha idadi ya migahawa, bazaar, maduka ya jadi ya ufundi, ukumbi wa michezo wazi na viwanja vya kufanyia sherehe na matukio.

Hali ya maonesho ya makumbusho ya Sharm El-Sheikh inahusika na kuibuka na maendeleo ya ustaarabu wa Misri, na vile vile inatoa mwanga  kwenye mtu wa Misri na tabia yake kwa mazingira yanayomzunguka, na jinsi ya kuishi pamoja na viumbe vyake ambavyo  alivitakasa.ambapo Makumbusho yaonesha vitu 5,200 vilivyochaguliwa, vilivyochaguliwa kwa uangalifu kutoka kwa maduka ya makumbusho huko jumba la Manial , Kom Oshim, Saqqara, Makumbusho ya Suez, Ismailia na Greco-Roman huko Alexandria, Na Jumba la Makumbusho la Wamisri huko Tahrir, pamoja na maduka ya jiji la Luxor na Ashmounin huko Minya na mengineyo, yataonyeshwa ndani ya kumbi mbalimbali za jumba la makumbusho, yaani Jumba Kubwa, ukanda wa Hathor, eneo la makaburi, au nje. eneo la maonesho.

Ukumbi mkuu  unaonesha binadamu na wanyamapori katika Misri ya kale, kwa kuonyesha idadi ya picha za uchoraji zinazowakilisha familia ya Misri katika hatua tofauti za kihistoria. Pia inajumuisha kikundi cha sanamu za sphinx zinazowakilisha mwili wa wanyama na wanadamu, na sanamu ya mtu karibu na binti yake mdogo, pamoja na idadi ya wanyama watakatifu.Katika Misri ya kale, kama paka na kovu za maumbo na ukubwa mbalimbali, ambazo ziligunduliwa mwaka wa 2019 katika eneo la mambo ya kale ya Saqqara.

Ama kuhusu ukanda wa Hathor, uliitwa kwa jina hili kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya vipande vya mungu Hathor, pamoja na baadhi ya sanamu za wafalme Thutmose I, Hatshepsut, Nectanabo, Ramses II, na Ramesses III. Pia huonesha uigaji wa kaburi kamili la zamani na maelezo yake yote na yaliyomo ya samani za mazishi.

Miongoni mwa mabaki muhimu zaidi katika jumba la makumbusho ni kipande cha nadra cha mosaic kutoka Alexandria kilichoanzia karne ya nne KK, na sanamu ya mungu “Eros” wa kuwinda swala , ambayo inaonyeshwa kwenye mlango wa makumbusho, na sanamu nyingine adimu. ya mungu “Bas” iliyotengenezwa kwa udongo ambao haujakamilika ambao unaonyeshwa ndani ya ukumbi mkubwa, hii Mbali na vipande vipya vilivyogunduliwa katika baadhi ya maeneo ya kiakiolojia, kuonyeshwa kwa mara ya kwanza, kwa njia ya kuimarisha mfumo wa maonesho ya makumbusho.

Jumba la makumbusho pia linaonesha vitu 10 vya zamani kutoka kwa hazina za Mfalme Tutankhamun, kabla ya kuonyeshwa kwenye Jumba la Makumbusho Kuu la Misri.Sanamu ya Ka, sawa na Mfalme Tutankhamun, iliyofunikwa na resin nyeusi na kuvaa mongoose kichwani, ilichaguliwa kuwa kipande kikuu cha maonyesho,Hiki ni kivutio kwa wageni wanaotembelea jiji hilo kuona sehemu ya hazina za mfalme huyo mchanga kwa mara ya kwanza, na njia ya watu wenye mahitaji maalum imeanzishwa katika jumba la makumbusho.

Msikiti wa Maswahaba

Katika eneo la takriban mita elfu tatu katikati ya eneo la soko la zamani huko Sharm El-Sheikh, “Mji wa Amani” unaofuata mkoa wa Sinai Kusini, Msikiti wa Maswahaba uko katika mtindo wa kipekee wa usanifu ambao unachanganya. mila, anasa na historia, unaoangazia pwani ya Bahari Nyekundu na nyuma yake mlima, kama kwamba kutoka kwa moja ya hadithi za kale “Usiku Elfu Moja na Moja”  inachukuliwa kuwa “ikoni ya kipekee” katika usanifu wa kisasa wa Kiislamu. Idadi kubwa ya watalii kutoka mataifa mbalimbali humiminikia humo kuuliza maswali kuhusu Uislamu, kwani una nafasi muhimu katika kurekebisha dhana potofu katika dini ya Kiislamu, na kubadilisha Taswira ambayo baadhi ya mataifa wanayo kuhusu Uislamu, na kueneza hakikisho katika nyoyo za kila anayezuru Misri.

Bustani ya Amani

Bustani ya Amani au Bustani ya Kimataifa ya Mimea iko huko Sharm El-Sheikh kwenye eneo la ekari 33, na ina aina 37 za mimea ya dawa adimu.

Aikoni ya amani

Ni mnara wa ukumbusho ulio katikati ya uwanja wa Al-Salam, ambao ni mita 36,000, kwenye lango la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sharm El-Sheikh, Barabara ya Dahab, na barabara ya pete ya Sharm El-Sheikh. Aikoni imeundwa kwa namna ya makundi ya granite nyeusi iliyoshikilia majani ya lotus, yamezingirwa na mabawa manane zilizochochewa na mabawa ya Ra yenye kipenyo cha mita 10, ambayo juu yake kuna ramani ya ulimwengu iliyotengenezwa kwa chuma cha pua, ina tovuti ya Misri kwa rangi ya dhahabu. na njiwa wakiruka juu yake wakiwa wamebeba tawi la mzeituni kama ishara ya amani.

Aikoni hiyo iliundwa na kubuniwa na mikono ya Wamisri kama ishara ya amani, na ilisajiliwa katika Kitabu cha Rekodi cha Guinness kama kazi kubwa na ndefu zaidi ya sanaa ya chuma Duniani.

Kanisa la Mbinguni

Ni kubwa zaidi kati ya makanisa ya Sinai, na makao yake makuu yako katika mtaa wa Al-Nour huko  Sharm El-Sheikh. Msingi wa kanisa uliwekwa na Papa Shenouda III, Papa wa Aleksandria na Patriaki wa Jimbo la Mtakatifu Marko mwaka 2002, Na aliizindua tarehe tano Disemba 2010, kwa gharama ya jumla ya pauni milioni 100 za Misri.

Vyanzo

Tovuti ya Wizara ya Mazingira ya Kimisri.
Tovuti ya Taasisi kuu ya Taarifa.
Tovuti ya Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale.

Check Also
Close
Back to top button