Habari Tofauti

MAMA MARIAM MWINYI AZINDUA KAMBI  YA MATIBABU NA UPASUAJI BURE KWA WANANCHI  ZANZIBAR

0:00

Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu, na Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mhe.Mama Mariam Mwinyi ametoa shukrani kwa uongozi wa Hospitali ya Kitengule , Tanlink Medical Tourism Agency na wadau mbalimbali kwa kuandaa na kuratibu zoezi la utoaji wa huduma za afya za kibingwa ambazo zinatolewa bure kwa wananchi wa Zanzibar .

Mama Mariam Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 05 Septemba 2023 akizindua kambi maalumu ya matibabu na upasuaji iliyoandaliwa na Hospitali ya Kitengule, Tanlink Medical Tourism  Agency kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Zanzibar pamoja na Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF)  katika  Hospitali ya Wilaya ya Kusini, Kitogani Mkoa wa Kusini Unguja .

Aidha, Mama Mariam Mwinyi amesema ni hatua muhimu kufanyika zoezi hilo katika kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi kwa kuimarisha huduma za afya na kuzisogeza karibu kwa wananchi.

Back to top button