Watawala Wa Misri

Khedive Abbas Helmy

Abbas Helmy II, mwana wa  Mohammed Tawfiq Pasha, mwana wa Ismail, mwana wa Ibrahim,  mwana wa Mohammed Ali.

Alizaliwa mnamo Julai 14, mwaka 1874 ndani ya Ikulu ya Qoba na mama yake ndiye ni Malkia Amina Hanem, mwana wa Ibrahim Elhami ambaye ni mwana mkubwa zaidi miongoni mwa wana wa Khedive Tawfiq.

Alisomeshwa na waalimu maalum katika shule ya Wungawana mjini Kairo, iliyoanzishwa na Baba yake ndani ya Ikulu hadi akiwa na miaka 10 , halafu alipelekwa huko Switzerland kwa ajili ya kusoma ambapo alifunzwa katika shule ya “Thod Yakom” huko Geneva mnamo kipindi cha kati ya 1883 hadi 1887 na pia kituo cha “Tarz Yanom” huko Vienna mwaka wa 1888 , ambapo ni shule iliyoanzishwa kwa ajili ya kuwaelemisha wana wa tabaka la Wungawana wa Austria na Hungary , ambapo mtawala Tawfiq alikuwa na hofu ya kumfundisha huko Uingereza na Ufaransa kutokana na tamaa zao za kuikalia Misri.

Na ghafla Baba yake alifariki Dunia na yeye bado ni mwanafunzi huko Vienna , na tayari alielekea Misri na zama yake ilianza wakati wa kuwa na miaka 18 kulingana na kalenda ya Kiislamu , na alishika madaraka ya Misri siku moja tu baada ya kifo cha babake mnamo Januari 8, 1892 , na alifika mkoa wa Alexanderia halafu Kairo mnamo Januari 16, 1892 na alianza kujali mambo ya utawala , kisha Lord Kromer mtawala wa ukoloni wa Uingereza nchini Misri alimwambia kuwa yeye “Mmisri Kabisa” .

kisha Khedive Abbas Helmy II alikuza mahusiano yake na jeshi , na  alitoa amri kwa  kupandisha cheo maafisa wengi wamisri ,
Na alikuwa anahudhuria majadiliano ya kijeshi,pia alikuwa amekagua vituo vya kijeshi , na magazeti mengi yalijitokeza ndani ya zama yake kama vile : Gazeti la Elhelal mwaka wa 1892 , Lewaa 1900  na Aljarida mwaka wa 1907.

Na pia Jumuiya ya Kiislamu ilianzishwa wakati wa enzi yake kwa lengo la kuwaangalia kwa ukaribu  wamaskini na kusambaa elimu mnamo 1892.

Miji ya Kimisri ilihusika sana na Reli , na tena Reli zilianza kupanua ambapo ndani ya mwaka wa 1893 kituo cha reli kilizinduliwa kati ya mji wa Asyut na Gerga , na pia kutoka mkoa wa Ismailia hadi Port Said  na reli nyingine nyingi.

Khedive huyo alitoa sheria ya marekibisho ya Al_Azhar ikijumuisha vifungu (62).

Sudan ilirejeshwa, Wakati wa utawala wake,ambapo Cromer alimwambia Khedive huyo kuhusu kujiandaa kwa kuunda kampeni ya kuelekea Sudan mnamo Machi 13 mwaka wa 1869, na makubaliano ya utawala wa pamoja kwa Sudan yalifanyika kati ya serikali ya Misri na Uingereza mwaka wa 1899.

Mwaka wa 1898,alianzisha benki ya Al_Ahly ya Misri, Jumuiya ya kilimo mwaka huo huo, na Benki ya Mali isiyohamishika ya Misri mwaka wa 1902.

Al Qanatter_El Khairya ilirekebishwa Wakati wa utawala wake, na zingine zilijengwa karibu nao zilizoitwa, “Mohamed Ali” na alianza kufanya kazi kwenye Bwawa la Aswan mwaka wa 1898, na alimaliza mwaka wa 1902 na Qanater Assiyut ,Qanater Esna ilianzishwa mwaka wa 1908, na hifadhi ya Aswan hupanda juu kwa mara ya kwanza mwaka wa 1912.

Mwaka wa 1908 ,alianzisha daraja la Abbas (sasa Giza),daraja la mfalme Saleh,na daraja la Mohamed Ali, kisha alianzisha daraja la Bulaq,na daraja la el Zamalek mwaka wa 1912,kisha daraja la el galaa mwaka wa 1914 na madaraja mengine.

Elimu wakati wa utawala wake ilipiga hatua, kamati iliundwa kwa uongozi wa mwenyekiti mmoja ili kukusanya michango ya misheni za kisayansi nje ya nchi iliyojumuisha wanafunzi wakumi, thamani ya mischango ilifika Paundi elfu tano, lakini imeamuliwa kuweka kiwango hiki kwa ajili ya mradi wa chuo kikuu cha taifa ambao ulishinda kikamilifu,na ulifunguliwa mwaka wa 1908, na mfalme Abbas Helmy alituma misheni ya kwanza ya kisayansi nje ya nchi.

Alianzisha barabara ya kilimo iliyounganisha Kairo na Alexandria mwaka wa 1912, na nyingine iliyounganisha Helwan na Kairo, kisha na Al_Qanater el Khairya.

Petroli iligunduliwa wakati wa utawala wake mwaka wa 1912.

  Jumuiya ya Kutunga Sheria ilianzishwa wakati wa utawala wake mwaka wa 1914.

Mfalme alitetea haki za Misri, na alipingana na sera ya Uingereza ,alitaka kuwa mtawala mwaminifu sio mwanasesere mikononi mwa Waingereza ,alijaribu kufuata  sera ya mageuzi na kuwa karibu na wamisri na kupinga ukoloni wa Uingereza,lakini hakudumu kwa muda mrefu.

Waingereza walitumia fursa ya kuzuka vita vikuu vya kwanza,hivyo wakamuondoa madarakani Desemba 19 mwaka wa 1914,na wakati huo alikuwa nje ya nchi, hivyo wakamuoma kutorudi, kisha wakamuweka mjomba wake. Hussein Kamel kama sultani wa Misri.

Alifariki Dunia Desemba,19 mwaka wa 1944.

Check Also
Close
Back to top button