Siasa

Rais El-Sisi athibitisha kwamba Umoja imara wa kitaifa unaowaunganisha Watu wa Misri ni nguzo yetu kuu ya Ustawi na Maendeleo

Ali Mahmoud

0:00

Rais Abdel Fattah El-Sisi amepeleka pongezi kwa utakatifu wa Baba Tawadros wa Pili Baba wa Alexandria, Patriaki wa Jimbo la Mtakatifu Marko wakati wa kusherehekea Krismasi Njema.

Rais El-Sisi alisema katika pongezi yake: “Utakatifu wa Baba Tawadros wa Pili, Baba wa Alexandria, Patriaki wa Jimbo la Mtakatifu Marko, ni furaha kwangu kutuma kwa utakatifu wako na kwa ndugu zangu na wana wangu, wakristo wa Misri, pongezi zangu za dhati na matakwa bora kwa mnasaba wa kusherehekea Krismasi Njema, Mwenyezi Mungu airudi kwenu kwa mema na baraka”.

Rais aliongeza: “Katika sherehe hiyo nzuri, ningependa kusifu Umoja imara wa kitaifa unaowaunganisha wana wa nchi hii kubwa katika historia yote, kwani Misri ni chimbuko la Jumbe za Mbinguni na ni hazina ya Mwenyezi Mungu katika nchi yake na kwamba umoja wetu wa kitaifa ndio nguzo yetu kuu ya ukuzi na maendeleo, na namuomba Mwenyezi Mungu aihifadhi Misri na kuwatunza watu wake, na adumishe baraka ya udugu miongoni mwa wana wake wote, Waislamu na Wakristo, na atufanyie mema kwa ajili ya watu hawa wakubwa wenye heshima, na mwanzoni mwa mwaka mpya ninawatakia ndugu wote wakristo mwaka mpya uliojaa mafanikio, na Misri yetu iendelee, kukua, kufanikiwa na heri ya mwaka mpya”.

Rais El-Sisi alituma pongezi kwa wakristo wa Misri nje ya nchi, zilizowasilishwa na balozi zetu na kanseli zetu Duniani kote, akielezea matumaini yake kwao kwa Mafanikio endelevu, akimwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu aifanye sikukuu njema yenye furaha, kuirudisha kwao kwa heri yote, na kuibariki Misri yetu mpendwa kwa Maendeleo endelevu, Ukuzi na Ustawi.

Back to top button